Idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Idadi wa waliopotelewa na sajiliwa katika ofizi tezu katika kipindi cha ziara ya Arubaini ilifika 9869 na Sayyid Swafi asifu juhudi za watendaji wake…

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Faras Abbasi Hamza amesema kua, idadi ya watu walio potelewa katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), walio sajiliwa katika vituo vyetu vyote 43 vilivyopo katika barabara zinazo ingia Karbala walifika 9869, kati ya hao 3175 ni wale walio potezana na wenzao na 6694 ni wale waliopotea na wakakaa katika vituo vyetu kwa ajili ya kuwatafuta ndugu zao, ambapo watu 6661 tuliwakabidhi kwa ndugu zao, na walibaki 33 tukawakabidhi katika kituo cha malazi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa hiyo tulifanikiwa kuwakutanisha walio potea na ndugu zao kwa asilimia %99.

Akaongeza kua: “Kuwashughulikia walio potea ni jambo muhimu sana hususan watoto na wazee na lina thawabu nyingi, kwani ni sehemu ya kumsaidia mwenye shida, malipo yanaongezeka mara dufu anapokua mwenye shida ni zaairu wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), kwenye msongamano mkubwa kama huu watu kupotezana ni jambo la kawaida, hivyo anaweza akahangaika kumtafuta ndugu yake bila mafanikio”.

Akasema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu ilibeba jukumu la kuhakikisha inawakutanisha walio potezana, wamefanya juhudi kubwa sana katika kutekeleza swala hilo, ambapo utekelezaji wake ulihusisha vitengo mbalimbali vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile kitengo cha magodauni, utumishi, usimamizi wa kihandisi, habari, malezi na elimu, uchumi na vinginevyo, pia kulikua ushirikiano mkubwa na idara ya kumuelekeza zaairu ya Atabatu Husseiniyya tukufu ambao waliandaa muongozo wa kumtafuta aliye potea, pamoja na kitengo cha katikati ya haram mbili (maa baina haramain) na shirika la Alkafeel na ofisi ya mawasiliano ya wizara ya mambo ya ndani pamoja na vituo vya afya vya Karbala na shirika la (Irthalnak) la Intanet, kupitia muwakilishi wao wa Karbala, hali kadhalika tulishirikiana na kituo cha kuongoza walio potea cha Najafu, tambua kua mafanikio haya pia yalipatikana kutokana na kushirikiana kwa karibu kati ya idara ya mawasiliano na idara ya uhusiano na vyuo vikuu pamoja na kitengo kikuu cha mahusiano.

Muhandisi Faras akasema: “Huduma hii imeendelea kua bora kila mwaka baada ya kutoka katika hatua ya kufunga mahema hapa na pale hadi kufikia hatua hii ya kua na vituo maalumu zaidi ya (34) katika barabara za Najafi, Baabil, Bagdad na ndani ya mji wa Karbala, tena vilivyo na vifaa vya mawasiliano vya kisasa, kama vile kompyuta, screen, kamera na vinginevyo miongoni mwa mitambo ya kiteknolojia, pamoja na kua na nyubma za kulala walio potea iwapo watakaa zaidi ya saa 12 bila kukutana na jamaa zao, vituo hivyo vinaongozwa na wanafunzi wa vyuo katoka mikoa mbalimbali ya Iraq”.

Akabainisha kua: “Hakika idadi wa watu waliopotezana na kupotea katika ziara iliyo pita walikua elfu 17, idadi hiyo imepungua hadi kufika watu elfu 9869 katika ziara hii, kutokana na kuongezeka kwa uwelewa wa watu kuhusu namna ya kuamiliana na vituo hivi pamoja na kutumia njia za kisasa katika kutafuta walio potea pia kutengeneza vitambulisho (baji) kwa ajili vya kuwatambua watoto na wazee walivyo vaa mikononi kwao kama saa pamoja na kuimarika kwa ushirikiano wetu na mawakibu”.

Muhandisi Faras Abbasi Hamza amefafanua kua, hakika kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi chini ya usimamizi wake wa utendaji wa harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika ziara ya Arubaini na kusifu utendaji wa vituo hivi, kulitupa moya zaidi wa kuboresha huduma zetu. Mwisho wa maongezi yake; aliwaomba mazuwaru waliopotelewa na watoto wao waliopo hivi sasa katika nyumba za malazi wawasiliane nao kwa namba zifuatazo: (07602405888 au 007602405889).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: