Mchepuo wa elimu ya kiislamu katika chuo kikuu cha Karbala wategemea moja ya machapisho ya Atabatu Abbasiyya ya Qur’an kama kitabu cha kufundishia…

Maoni katika picha
Mchepuo wa masomo ya kiislamu katika chuo kikuu cha Karbala watumia kitabu kilicho andikwa na Atabatu Abbasiyya kiitwacho (Mwongozo wa mwanafunzi juzuu Wadhariyaat) kufundishia katika kitengo cha masomo ya Qur’an na Fiqhi hatua ya nne, kitabu hicho kilichapishwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Wamepasisha kutumia kitabu hicho baada ya kujiridhisha na ubora wa vitabu vinavyo andikwa na kituo cha maarifa ya Qur’an na kuifasiri katika kiwango cha sekula kutokana na ubora wa mada zake kuhusu Qur’an.

Mkuu wa mchepuo wa maarifa ya kiislamu amebainisha kua: “Selebasi hii inalenga kuongeza uwezo wa wanafunzi katika lugha na Qur’an, hivyo kulikua na uhitaji mkubwa wa kupata kitabu mnasaba kinacho weza kutumika katika vyuo vikuu vya Iraq, hususan vya kiislamu, kitabu kilicho na mafundisho sahihi ya Qur’an tukufu pamoja na sira ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s)”.

Kumbuka kua hiki ni miongoni mwa vitabu vya Qur’an vilivyo andikwa na kuchapishwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha katika Maahadi ya Qur’an tukufu, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya, kinaelezea kwa upana maswala ya Qur’an, kimepewa jina la (Mwongozo wa mwanafunzi) kimejaa riwaya nyingi za maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kinakubaliana na Qur’an tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: