Baada ya kumaliza kazi zilizo kua zinafungamana na ziara ya Arubaini, kitengo cha uangalizi wa haram tukufu chabadilisha zulia katika haram ya Abulfadhil Abbasi…

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa majukumu yake ya uangalizi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kitengo cha uangalizi wa haram tukufu chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kimebadilisha zulia lililo kuwa katika haram hiyo tukufu, baada ya kukamilisha majukumu yote kiliyo pewa katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Wafanyakazi wa kitengo hicho walikutwa wanafanya kazi ya kutandika zuria jipwa mida ya usiku, hufanya hivyo kwa ajili ya kuepuka msongamano wa watu katika mida ya mchana, kwani katikati ya usiku watu hupungua na kurahisisha ufanyaji wa kazi, kabla ya hapo walitandua mazulia yaliyo kuwepo na kuyafanyia usafi pamoja na kuyapulizia dawa ya kuzuia kuharibika.

Kazi hii ni miongoni mwa majukumu yake ya kila wakati na kila wanapo maliza ziara ya Arubaini hubadilisha mazulia, kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, zulia walilo tandika hivi sasa ni miongoni mwa mazulia bora zaidi, limetengenezwa na shirika la Raswinah walilo ingia nalo mkataba rasmi kwa ajili ya kazi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: