Katika kumbukumbu ya kufariki Mtume, Shule ya wasichana Sayyidul-Maa yafanya matembezi ya maombolezo ya wanafunzi na walimu…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Alkhamisi (26 Safar 1439h) sawa na (16 Novemba 2017m) Shule ya wasichana Sayyidul-Maa ambayo ipo chini ya kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya matembezi ya maombolezo yaliyo husisha wanafunzi na walimu.

Matembezi hayo yamefanyika kama sehemu ya kukumbuka kufariki kwa Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w), yalianzia shuleni hapo na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), kisha wakatembea hadi katika malalo ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipitia katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili na wakafanya majlis katika ukumbi wa haram ya Abbasi (a.s).

Kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya matukufu hupewa umuhimu mkubwa na kitengo cha malezi na elimu, kwani jambo hilo linasaidia kufungamanisha wanafunzi na turathi za Ahlulbait (a.s), na huzingatiwa kua ni miongoni mwa harakati muhimu za ziada, zinazo saidia kujenga kizazi kizuri kinacho pambika na akhlaqi za Ahlulbait (a.s). Tunatarajia jambo hili lizae matunda, tupate kizazi kinacho beba rikra za Ahlulbait (a.s) na kinacho watetea.

Fahamu kua matembezi haya ya wanafunzi yamefanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo, wakati wa matembezi hayo wanafunzi waliimba qaswida za kuomboleza na zinazo onyesha mapenzi yao kwa Mtume mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: