Ugeni kutoka chuo kikuu cha Kufa katika mchepuo wa udaktari, watembelea chuo kikuu cha Ameed kuangalia maadalizi ya mwaka mpya wa masomo, na wasisitiza kua maandalizi yanaendana na aina ya wanafunzi wanao pokelewa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ziara zinazo fanywa na wasomi wa kisekula wa ndani na nje ya Iraq, wanao kuja kutembelea chuo kikuu cha Ameed, hivi karibuni chuo hicho kimepata ugeni kutoka katika chuo kikuu cha Kufa mchepuo wa udaktari, wamekuja kuangalia maandalizi yanayo fanywa na chuo hiki ya kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo katika michepuo ya (Udaktari, Udaktari wa meno na Uuguzi).

Ugeni huo uliongozwa na rais wa chuo pamoja na baadhi ya viongozi, wametembelea madarasa na kuangalia vifaa vya kusomea pamoja na kupata maelezo kuhusu vifaa tiba na vifaa vilivyopo katika maabara.

Mkuu wa idara ya udaktari katika chuo kikuu cha Kufa dokta Wisaam Lamiy amebainisha kua: “Lengo la ziara yetu ni kuangalia maandalizi yanayo fanywa na chuo cha Ameed, tumetembelea madarasa na kubaini kua maandalizi yao ni mazuri sana, pia wana vifaa bora vya kusomea na maabara nzuri”.

Makamo mkuu wa idara ya udaktari katika chuo kikuu cha Kufa dokta Haidari Adhariy aliongeza kusema kua: “Hakika maandalizi ya kimkakati kuhusu maswala ya kupokea wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo, kumbi za kusomea na vifaa vya maabara, vipo katika ubora wa hali ya juu, wamejiandaa kupokea wahitimu wa shule za upili (sekondari), hakika wanafunzi hao wanaendana vilivyo na madarasa haya, maandalizi ya aina hii husaidia kuongeza kiwango cha ufaulu”.

Fahamu kua chuo kikuu cha Ameed kiliingia mkataba na mchepuo wa udaktari katika chuo kikuu cha Kufa, na wanatumia selibasi moja ya masomo, ambayo ndio selebasi tegemezi katika chuo kikuu cha Lestar cha Ungereza.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesha kamilisha maandalizi ya kupokea wanafunzi katika michepuo yake mitatu (Udaktari, Udaktari wa meno na Uuguzi) kwa mwaka mpya wa masomo 2017 – 2018 chini ya taratibu na kanuni za wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: