Kikosi cha Abbasi (a.s) chakamilisha maandalizi ya vita ya kukomboa kisiwa kikubwa…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kukamilisha maandalizi ya vita ya kukomboa kisiwa kikubwa (Jaziratu Kubra) kinacho unganisha baina ya mkoa wa Mosul, Swalahudin na Anmbaar, na kusafisha kabisa mabaki ya magaidi wa Daesh walio kimbia vitani na kikifanya kisiwa hicho kua maficho yao wakiogopa kukabiliwa na majeshi ya ukombozi, jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi walio washushia kipigo.

Kiongozi wa kikosi hicho Shekh Maitham Zaidiy amebainisha kua: “Hakika vita hii itatekelezwa na wale walio itikia wito wa jihadi ya kutoshelezeana (kifaaiy) miongoni mwa wazalendo wa Hashdi Sha’abiy, akasema kua; kikosi hiki kitapigana upande mmoja kati ya pande za vita hiyo, maandalizi ni ya hali ya juu na kuna mambo mapya ya kushitukiza tutakayo tangaza katika vita hii ambayo tunatarajia kumaliza ukurasa wa magaidi katika nchi hii kipenzi, tumesha fanya vikao vya pamoja na viongozi wengine kwa ajili ya kuweka mikakati ya pamoja kuhusu vita hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: