Idara ya maji inatoa huduma kwa mawakibu za utumishi na waombolezaji katika kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w) katika mkoa mtukufu wa Najafu…

Maoni katika picha
Idara ya umwagiliaji (maji) chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wanatoa huduma kwa mazuwaru na waombolezaji wa kifo cha Mtume (s.a.w.w), wanao elekea katika kaburi la kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa mtukufu wa Najafu, kwa kugawa maji na barafu.

Kiongozi wa idara hiyo Ahmadi Hanun ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Idara yetu imejipanga kugawa maji kwa mazuwaru na mawakibu za kuomboleza wanao huisha kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w), katika malalo ya mtoto ya ammi yake na wasii wake Ali bun Abu Twalib (a.s), tulianza kufanya kazi hii toka siku mbili zilizo pita na bado tunaendelea, tumefanikiwa kugawa maji safi katika barabara ya Najafu – Karbala na tunatumia maukibu ya Ataba mbili tukufu kama kituo chetu cha kutolea huduma”.

Akaongeza kua: “Kazi yetu tumeigawa sehemu tofauti, sehemu ya kwanza ni kituo kikuu cha shughuli zetu ambapo ni katika maukibu ya Ataba mbili tukufu, upande wa Haidariyya hadi katika mpaka wa mkoa mtukufu wa Najafu, na sehemu nyingine ni makao makuu ya mji wa zamani na katika daraja la Thauratu Ishriin hadi katika uwanja wa kuaga (taudii) mkabala na barabara ya Shekh Tusi inayo elekea katika haram tukufu ya Alawiyya”.

Akabainisha kua: “Tulifanya maandalizi ya kutosha kama idara ya maji kwa ajili ya kuhudumia katika ziara hii, ugawaji wetu wa maji hauhusishi magari ya maji tu, bali tunagawa hadi maji ya kwenye grasi yanayo tengenezwa na kiwanda cha maji cha Ataba tukufu pamoja na barafu kutoka katika kiwanda hicho hicho, tunaanza kazi mapema asubuhi na tunafunga usiku mwingi”.

Kumbuka kua idara ya maji (umwagiliaji) ilifanya kazi kubwa katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), walihakikisha wanagawa maji safi ya kunywa kwa mazuwaru wote na mawakibu za utoaji wa huduma pamoja na vitengo vya Ataba, pia wanakazi nyingi za nje za kugawa maji kwa mazuwaru wanao kwenda katika Ataba zingine tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: