Miongoni mwa machapisho ya kituo cha kiislamu cha masomo ya mikakati ni jarida la sehemu za Aqida…

Maoni katika picha
Jarida la Aqida linalo chapishwa na kituo cha kiislamu cha masomo ya mikakati kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa machapisho yanayo kubalika na watu wa tabaka tofauti, linaandika maswala ya Aqida na fani za maneno ya zamani na yasasa, kwa kutegemia hoja za kiakili zinazo tokana na misingi ya uongofu wa vizito viwili, kwa ajili ya kuziba pengo lililopo katika maktaba za kiislamu kuhusu utafiti katika sekta hii, jarida hili linalenga mambo yafuatayo:

  • 1- Kufundisha Aqida na kuilinda.
  • 2- Kujibu shubha zinazo zushwa kuhusu dini ya kiislamu na madhehebu.
  • 3- Kuonyesha nafasi ya Aqida katika maisha ya kijamii.
  • 4- Kufungua mlango wa kuongea na kujadiliana.

Elimu ya Aqida pamoja na kukumbwa na mabadiliko ya selibasi katika historia ya elimu hiyo na kuichanganya na elimu zingine, kama vile falsafa na Irfaan kuliko fanywa na baadhi ya wanachuoni, pamoja na kudhihiri wingu jipya la mabadiliko, bado kuna umuhimu mkubwa wa kuliangazia somo hili katika mas-ala zake, selibasi zake na malengo yake, ukizingatia kua tunaishi katika zama za vita ya kielimu, zama ambazo zimezushwa shubha nyingi kuhusu dini, kutokana na umuhimu huo ndipo likaja wazo la kuanzishwa kwa jarida la (Aqida), ili liangazie mas-ala ya elimu ya maneno na Aqida, kwa kuzingatia hoja za kiakili zinazo tokana na uongofu wa vizito viwili alivyo tuachia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa ajili ya kulinda umma usipotee, na ili kuziba mwanya uliopo katika maktaba za kiislamu kupitia tafiti za wanachuoni wetu watukufu.

Jarida hili la (Aqida) linahimiza kua na kauli moja na kusimama imara mbele ya adui, kwa kuamini uwezekano wa kuishi kijamii na kuwa na kauli moja za wanasiasa pamoja na kutofautiana kwa imani zao, kwa kufuata mwongozo ulio asisiwa na kiongozi wa waumini (a.s) alipo sema: (Watu.. wapo makundi mawili: Imma ni ndugu yako katika dini, au ndugu yako katika uumbwaji –ubinadamu-).

Nafasi ya Aqida ni nafasi ya kutafakari na kuongea, na nafasi ya jamii ni nafasi ya undugu na kuishi kwa amani sambamba na kutumia maneno mazuri tunapo ongea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: