Kwa kushiriki kikosi cha Abbasi; vita ya kukomboa jangwa la kisiwa kikubwa yaanza…

Maoni katika picha
Katika asubuhi ya kwanza majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanaandika historia mpya kwa kuvamia ngome (vizuizi) vya kuingia katika eneo la kisiwa kikubwa, katika opresheni ya kukomboa miji ya kisiwa hicho inayo pakana na Swalahu-Dini, Nainawa na Ambaar kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh, wakisaidiana na ndege za kivita za jeshi la serikali ya Iraq, sambamba na kikosi cha mizinga na mabomu cha wapiganaji wa kikosi cha Abbasi, wametoa kipigo kikali kwa mabaki ya magaidi ya Daesh.

Kwa mujibu wa taarifa za kikosi hicho, wapiganaji wamefikia malengo yao kwa kiwango cha juu na wamefanikiwa kukomboa vijiji viwili (Burait na Samnu), wakaendelea na kukomboa vijiji vingine viwili (Sheikhaan na Shaikha), na wamedhibiti kituo kikuu cha mawasiliano pamoja na kuteka idadi kubwa ya magari ya magaidi ya Daesh baada ya magaidi hao kukimbia.

Kwa ufupi eneo lililo kombolewa na kikosi cha Abbasi (a.s) katika siku ya kwanza ya vita ya kukomboa kisiwa kikubwa ni kilometa 35.

Kumbuka kua viongozi wa kijeshi wanao ongoza opresheni hii wametangaza Alkhamisi ya leo (23 Novemba 2017m) kuingia hatua ya pili ya vita ya kukomboa maeneo yanayo pakana na Swalahu-Dini, Nainawa na Ambaar kwa ushirikiano wa jeshi la serikali ya Iraq na Hashdi Sha’abi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: