Atabatu Abbasiyya tukufu yatembelea vikosi vya jeshi vilivyopo katika mpaka wa Sirya na Iraq pamoja na mji wa Hadhar…

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio husisha wafanya kazi na mashekhe kutoka katika kitengo cha dini, wameenda kutoa msaada wa kimkakati kwa wapiganaji wa jeshi la serikali na vikundi vya Hashdi Sha’abi waliopo katika mpaka wa Sirya na Iraq, pamoja na mji wa Hadhar na uwanja wa ndege wa Tharya karibu na mji wa Qirwaan, na kuwapa baadhi ya mahitaji muhimu, kama vile chakula, mavazi ya baridi na mablangeti.

Shekh Haidari Aaridhiy kutoka katika kitengo cha dini aliye ongozana na msafara huo amesema kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi, na ukiwa ni muendelezo wa kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu za kutoa msaada wa kimkakati kwa wapiganaji wetu katika miaka yote ya vita dhidi ya magaidi wa Daesh, tumeenda kutembelea vikosi vya jeshi vilivyopo katika mpaka wa Iraq na Sirya, pamoja na mji wa Hadhar na uwanja wa ndege wa Tharya na kuwapa mahitaji muhimu yatakayo wasaidia katika kipindi hiki cha baridi”.

Akaongeza kusema kua: “Ziara yetu haikuishia hapo tu, wapiganaji wetu walishiriki kukomboa kisiwa cha China na tumekua tukitoa msaada wakati wote wa vita ya kukomboa aridhidhi ya Iraq, pia tumewatembelea watu waliopo katika vikundi vya Husseiniyya vinavyo toa msaada kwa wapiganaji na kutoa msaada kwao”.

Shekh Haidari Aaridhiy ameonyesha umuhimu wa kutoa msaada wa kimkakati kwa wapiganaji akisema kua: “Kila mtu anayo nafasi ya kushirikiana na wapiganaji katika uwanja wa vita, hakika mwanafunzi wa hauza anawakilisha nafasi ya Marjaa dini, anapo beba siraha pamoja na wapiganaji tende hilo huongeza morari (ari) kwa wapiganaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: