Chuo cha Qadisiyya ni moja ya vituo vya kutambulishia utunzi bora kuhusu Qur’an tukufu kwa mujibu wa vizito viwili…

Maoni katika picha
Utambulisho wa utunzi bora kuhusu Qur’an tukufu kwa mujibu wa vizito viwili uliofanywa na kitengo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umepita katika hatua nyingi za utambulisho, vyuo vikuu vina nafasi kubwa katika hilo, na chuo kikuu cha Qadisiyya kilichopo katika mji wa Diwaniyya kimefanya nadwa ya utambulisho iliyo simamiwa na mkuu wa kitengo hicho, Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidiy.

Nadwa ilifanyiwa katika ukumbi wa kitivo cha malezi, ilipata mahudhurio makubwa ya walimu na wanafunzi wa kitivo hicho pamoja na wa kitivo cha lugha na wageni waalikwa, Shekh Zubaidiy alielezea vipengele muhimu vya mwenendo wa haki wa vizito viwili, akazungumzia nafasi ya akili katika kun’gamua (kuujua) ukweli huu pekee unao weza kumuokoa mtu kutoka katika upotevu, kisha akatambulisha mashindano yatakayo endeshwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, ambayo mwisho wa kupokea washiriki wa mashindano hayo utakuwa ni mwisho wa mwezi wa tano mwakani, wahudhuriaji wa nadwa walitoa michango yao na kuuliza maswali, naye Shekh Zubaidiy alitoa ufafanuzi na kujibu maswali yao.

Kumbuka mashindano hayo yanalenga kusambaza utamaduni halisi wa Qur’an kwa mujibu wa vizito viwili (Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu) katika jamii ya kiislamu kama alivyo husia Mtume (s.a.w.w).

Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano na mashariti yake angalia linki hii: https://alkafeel.net/ar-news/index?id=3627
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: