Ratika ya ufungaji wa kongamano hilo ilifanyika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na ilitanguliwa na vikao viwili vya kiutafiti, kikao cha kwanza kilifanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) chini ya usimamizi wa dokta Fatuma Salami na dokta Nuru Saidiy na walipitia kwa muhtasari tafiti (12), na kikao cha pili kilifanyika katika ukumbi wa Imamu Qassim (a.s), chini ya usimamizi wa dokta Ibtisaam Madaniy na dokta Zaharaa Mussawiy pia walipitia tafiti (12).
Mada zilizo tolewa katika vikao hivyo zilikua ni za kukamilisha zile zilizo tolewa jana asubuhi na jioni katika Atabatu Husseiniyya tukufu, zote zilipasishwa na kamati inayo husika na kupasisha tafiti.
Ratiba ya ufungaji wa kongamano ilifunguliwa kwa Qu’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha maalumu kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kisha likafuatia neno la ukaribisho kutoka kwa kiongozi wa idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Ustadhat Ashwaaq Abdul-Amiri, ambaye aliwakaribisha wahudhuriaji wote na washiriki wa kongamano hili walio kua nao kwa siku mbili, na akawasifu walio andika tafiti kutokana na juhudi zao zilizo onyesha uwezo wa wanawake wa kiislamu katika sekta ya elimu, pia akaelezea kuhusu kumbukumbu ya kutawazwa kwa Imamu Hujjah (a.f) na umihimu wa matukio haya katika nyoyo za waumini.
Akaongeza kusema kua: “Kongamano hili limekua na mafanikio makubwa katika sekta zote, tafiti zake za kielimu zimegusa mambo mengi na zimeandaliwa na kuwasiliswa vizuri”.
Halafu dokta Nuru Saidiy akaelezea matokeo na mapendekezo ya kongamano kama ifuatavyo:
- 1- Kupitia kongamano hili tumeweza kuonyesha picha ya mwanamke katika tukio la Karbala kwa kuelezea ushiriki wake katika mambo tofauti.
- 2- Msisitizo kuhusu umuhimu wa kuwasiliana na kushirikiana baina ya Ataba tukufu.
- 3- Umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika sekta tofauti za kielimu.
- 4- Umuhimu wa kuwasiliana baina ya watafiti walioshiriki katika kongamano.
- 5- Umuhimu wa Ataba na taasisi za kidini kunufaika na watafiti wa kike katika sekta mbalimbali za kielimu na kitamaduni.
- 6- Umuhimu wa kufanya makongamano kama haya mara kwa mara chini ya utaratibu maalumu.
Katika ratiba hii pia ilionyeshwa video ya harakati za wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na mwisho wa kongamano viligawiwa vyeti vya ushiriki kwa watu wato walio hudhuria katika kongamano hili, pamoja na kutoa zawadi kwa waliochangia kufanikiwa kwa kongamano hili.