Wataalamu wa kigeni na wa kiiraq kwa kutumia mitambo ya kisasa: Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua kituo maalumu cha kutibu meno…

Maoni katika picha
Katika juhudi ya kuhakikisha wanatoa huduma bora za matibabu kwa wakazi, zinazo endana na huduma za kimataifa, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua kituo maalumu cha kutibu meno katika mkoa wa Karbala kwa jina la (Kituo cha Lebanon cha tiba ya meno na usafi), kikiwa na madaktari bingwa kutoka Lebanon wakisimamiwa na mtaalamu raia wa Iraq, ili kufahamu zaidi kuhusu kituo hiki na huduma zake, mtandao wa Alkafeel ulikitembelea na kukutana na msimamizi mkuu wa kituo hicho dokta Muammar Aarajiy ili atuelezee huduma kuu zinazo tolewa na kituo hiki, naye alikua na haya ya kusema: “Sekta ya tiba ya meno hapa Iraq inapiga hatua kwa kasi sana, na wanatumia vifaa tiba vya kisasa kabisa na vimethibitisha mafanikio, mkoa wa Karbala ulikua na haja kubwa ya kupata kituo kama hiki, sasa kimefunguliwa tena chini ya usimamizi makini wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ilitutaka kufanya mradi huu”.

Akaongeza kusema kua: “Tunatarajia kutoa huduma bora za matibabu, zinazo fanana na zilizopo katika nchi jirani zilizo bobea katika tiba za meno na maswala yote yanayo husiana na meno, kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa zaidi na madaktari mahiri, hakika kituo hiki kimepambwa na vifaa tiba vya kisasa kabisa katika sekta ya tiba ya meno”.

Dokta Muammar akabainisha kua: Kituo kina vitengo vifuatavyo:

  • 1- Kitengo cha opreshen ya mdomo na meno.
  • 2- Kitengo cha opreshen.
  • 3- Kitengo cha tiba.
  • 4- Kitengo cha upimaji.
  • 5- Kitengo cha tiba ya meno.
  • 6- Kitengo cha tiba ya meno ya watoto.

Vitengo hivyo vinatoa huduma zifuatazo:

  • - Kusafisha mene (kuyafanya yawe meupe).
  • - Kupandikiza meno (meno bandia).
  • - Kutengeneza meno.
  • - Kutibu mizizi ya meno.
  • - Kuweka meno ya moja kwa moja na yale ya kuweka na kutoa.
  • - Kupendezesha uso (muonekano).

Fahamu kua kituo hiki kipo katika mkoa wa Karbala, barabara ya Sanatir karibu na daraja la Dhariba katika jengo la Dola Santar, na kinafanya kazi siku zote za wiki.

Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo: (07730170707 / 07807070170).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: