Katika mwenendo wa vizito viwili na kwa kusaidiana na walimu wa Hauza: Atabatu Abbasiyya tukufu yaendesha darasa mjadala la kitafiti…

Maoni katika picha
Mwendelezo wa kufanya tafiti kuhusu Qur’an, kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinaendesha ratiba ya darasa mjadala (nadwa) lenye anuani isemayo (Hadithi ya vizito viwili na athari yake katika tafsiri ya Qur’an tukufu) kwa kushirikiana na jopo la walimu wa hauza ya Najafu pamoja na watalamu wengi walio bobea katika fani hiyo na wanafunzi wa masomo ya dini kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Mkuu wa ratiba hii Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidiy kiongozi wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha ametuambia kuhusu ratiba hiyo kua: “Toka kuanza kazi kwa kituo chetu kimeweka vipawa mbele muhimu, miongoni mwa vipawa mbele hivyo ni kutilia umuhimu mwenendo wa vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu kama vinavyo elezewa na Qur’an tukufu, na kimetumia uwezo wake wote katika kutoa elimu kuhusu kuelezea mwenendo huo, na miongoni mwa juhudi hizo ni hizi darasa mjadala, makongamano na mashindano pamoja na machapisho mbalimbali, hata darasa mjadala hili ni miongoni mwa juhudi hizo”.

Akaongeza kusema kua: Ratiba hii inahusisha kufanya darasa mjadala kila siku ya Alkhamisi katika ukumbi wa Imamu Qassim ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na watakua wanakaribishwa viongozi na walimu wa hauza wenye elimu kubwa kuhusu mas-ala ya Qur’an, ili waweze kutoa michango yao katika kujadili swala la (Hadithi ya vizito viwili na athari yake katika tafsiri ya Qur’an tukufu), katika vikao hivi, anashiriki pia Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashkuri ambaye ni miongoni mwa walimu wa kubwa katika hauza ya Najafu”.

Shekhe Dhiyaau akasisitiza kua: “Hakika darasa mjadala hizi zitaendelea kwa miezi kadhaa kama zilivyo pangwa, na kituo kitaandaa na kuchapisha tafiti hizi kwa ajili ya kuitumikia Qur’an ba kizazi kitakasifu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: