Kuanza kwa hatua ya pili ya kukarabati na kuweka dhahabu katika jengo ambalo ndani yake ipo kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ametangaza kuanza kwa hatua ya pili ya mradi wa kukarabati ukuta na kuweka dhahabu katika eneo la ukuta wa dhahabu linalo julikana kama (Twaarimah), ambalo linajumuisha mlango mkuu unao elekea katika haram tukufu na kuangaliana na mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kukamilika hatua ya kwanza iliyo husisha sehemu za pembeni ya mlango huu upande wa kushoto na kulia.

Akaongeza kusema kua: “Hatua hii inakamilisha hatua iliyo tangulia na itazidisha uzuri katika Ataba tukufu na kulinda uimara wa ukuta na kuufanya udumu zaidi ukiwa katika muonekano ule ule bila kupoteza uzuri wake, chini ya usanifu bora wa kihandisi ulio pasishwa”.

Swaaigh akaongeza kusema kua: “Kazi muhimu zitakazo fanywa katika hatua hii ni kubadilisha tofali za zamani zilizopo katika ukuta wa mlango, hatua hii ni muhimu sana, kwa sababu tofali zilizo tumika zamani ni za ugongo ndio pia zilizopo katika msingi, kiasi hazina tofauti tena na tabaka lingine la udongo na zinasababisha unyevunyevu katika ukuta, unyevu nyevu huo unaleta madhara kwenye ukuta, pia madhara yake yamefika hadi katika tabaka iliyo wekwa dhahabu, ambapo inapata kutu na kuifanya kua nyeusi”.

Akabainisha kua: “Mafundi wetu watatoa tofali za zamani zilizo wekewa dhahabu juu yake, na kuweka mpya pamoja na kukarabati sehemu zote zenye mipasuko, na kuhakikisha wanajenga ukuta imara wenye upana unao endana na ukarabati huo, utaonganishwa na vipande maalumu vya chuma ili kuufanya kua kama ukuta mmoja, pamoja na kuongeza baadhi ya vitu vinavyo saidia kushikamana kwa ukuta na kuufanya kua na uwezo zaidi wa kubeba paa na vitu vtote vilivyopo katika paa”.

Kumbuka kua mradi huu unatekelezwa kutokana na utafiti mwingi uliofanywa na watalamu walio bobea katika fani hii, walifanya utafiti na kupima uwezo wa ukuta za Twarimah na nguzo zake wa kubeba paa mpya ya sasa, ndipo ikabainika kua ukuta huo hauna uwezo wa kubeba paa hiyo, baada ya kubaini hilo kazi ikagawanywa katika hatua tofauti, hatua ya kwanza ilikua ya kujenga nguzo, kisha ukajengwa ukuta hadi katika lango kuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: