Kwa muda mfupi na kwa kukidhi vigezo vya kiufundi: Watalamu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakamilisha mradi wa maji katika majengo ya makazi ya Abbasi…

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa miradi ya kihandisi wamekamilisha mradi wa maji katika majengo ya makazi ya Abbasi (a.s), ambayo ni majengo maalumu kwa ajili ya kuishi watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa muda mfupi wakazi wa nyumba hizo wamepata neema ya maji baada ya kua usambazaji wa maji katika nyumba hizo ulitegemea zaidi maji mbadala.

Utekelezaji wa mradi huu umefanyika baada ya kua na makubaliano ya msingi na viongozi wenye dhamana katika ofisi ya mkoa mtukufu wa Karbala, baada ya kushindikana kutekeleza mradi huu kwa kuchukua maji yaliyopo katika kituo cha karibu na majengo hayo, imebidi kuchukua maji kutoka katika moja ya matengi yaliyopo katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya wa nje, uliopo katika barabara ya kwenda Najafu, kiasi ambacho zimewekwa bomba kwa urefu wa kilometa 7.

Hali kadhalika mradi umehusisha kutengeneza mahodhi ya chini yenye upana wa 120 mt 3, na urefu wa mt 10.5 na kina cha mt 2.4, pamoja na tenki imara la juu lenye upana wa 220 mt 3, na yamefungwa mashine zenye uwezo wa kusukuma maji kwa presha ya 4.2 hadi 5 na kuyasambaza katika nyumba hizo, sambamba na kupandisha maji katika matenki ya juu na mambo mengine yote ikiwa ni pamoja na kubalansi umeme, pamoja na sistim ya kutoa maji katika matenki ya juu na kuyasambaza katika majengo ya makazi kwa kutumia pampu 2. Utekelezaji wa mradi huu umefuata vigezo vyote vya uhandisi na umefanyika katika ubora wa juu kabisa, pia umekamilika ndani ya muda ulio pangwa ambao ni siku 28 tu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: