Kukamilisha tafsiri ya kwanza ya ziara mbalimbali kwa kiingereza katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Darul-Kafeel ofisi ya tarjama na usambazaji chini ya kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel katika kitengo cha elimu na utamaduni ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wametoa kitabu cha tafsiri za ziara za Ataba za Karbala tukufu pamoja na ziara zingine maalumu kwa lugha ya kiingereza.

Mkuu wa kituo hicho bwana Jasaam Muhammad Saidi ameeleza kuhusu kitabu hicho kua: “Kwa mujibu wa watalamu wa tarjama, hakika kitabu hiki ni cha pekee kwa namna maneno yake yanavyo oana na maneno ya Ahlulbait (a.s), ukilinganisha na vitabu vingine vya aina hii vilivyo tafsiriwa India, Pakistani na Uingereza, kwani vitabu hivyo vilivyo andikwa nje ya Iraq, vilitafsiriwa na watu ambao lugha zao mama zilikua imma ni Kiingereza au Kihindi au Ki-urdu na wakajifundisha lugha ya pili ya kiarabu, jambo lililo sababisha tafsiri zao kua na mapungufu makubwa katika maana za baadhi ya maneno, kutokana na kutokua na uwelewa wa kina wa lugha ya kiarabu, ambayo ndio lugha ya asili ya ziara hizo, ukizingatia kua maneno ya Ahlulbait (a.s) yamejaa balagha”.

Akasisitiza kua: “Wakati baadhi ya watarjum wa kituo cha Utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel, wana uwezo ambao hawana wale watarjum wa vituo vilivyo tarjum ziara hizo hapo awali, kazi hii imefanywa kwa umakini na mtarjum Hussein Muhsin Bazazi Mussawiy mwenye uzowefu wa miaka (53) katika kazi ya kutarjum kiarabu kwenda kiingereza, pamoja na umahiri wake wa kanuni za lugha ya kiingereza, huandika mashairi ya kiingereza kama anavyo andika mashairi ya kiarabu ambayo ndio lugha mama kwake, katika ufanyaji wa kazi hii alisaidiana na mtarjum Baraaq Abdul-Hassan, tarjama hii wameandika kwa umakini na ufanisi mkubwa wa kilugha, wamejitahidi katika kuchagua misamiati inayo oana na makusudio ya maasumu (a.s) yaliyopo katika nakala za asili za ziara hizo”.

Akaongeza kua: “Kazi hii wameifanya kwa miezi miwili, na ikapangiliwa na kuhaririwa na bwana Husaam Saadiy katika kurasa 96, kisha ikachapishwa na kituo cha Darul-Kafeel cha uchapishaji na usambazaji, ilikiweze kuwanufaisha makumi ya maelu ya mazuwaru wanao ongea kiingereza kila mwaka”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: