Kutoka katika shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, Sayyid Ashiqar: Tutamaliza maafa ya mazao kama jinsi wairaq walivyo wamaliza magaidi wa Daesh…

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Muhammad Ashiqar amesisitiza kua; kama ulivyo patikana ushindi na kukombolewa ardhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh na kumaliza maafa yaliyo ikumba Iraq pamoja na maeneo matukufu kwa juhudi za wanajeshi wetu na Hashdi Sha’abi, vile vile kutokana na juhudi za shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, tutamaliza maafa ya mazao yanayo sababisha kushuka kwa mavuno, tutalisaidia shirika ili liongeze uzajishaji wa bidhaa zake ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa na zina mchango mkubwa wa kuirudisha Iraq kua nchi ya viwanda kwa mikono na ujuzi wa raia wa Iraq.

Aliyasema hayo alipo tembelea makao makuu ya shirika hilo yaliyopo katika mkoa mtukufu wa Karbala, akaongeza kusema kua: “Tumetembelea shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, hakika shirika hili linamaendeleo makubwa katika sekta zake, linatengeneza bidhaa mbalimbali zinazo hitajiwa na watumiaji, katika sekta ya kilimo na viwanda, hakika sekta ya uzalishaji inafanya kazi inayo endana na maendeleo ya ulimwengu wa sasa na wanatoa bidhaa zenye ubora mkubwa”.

Akabainisha kua: “Jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba bidhaa zote zinatengenezwa na raia wa Iraq, wafanya kazi wa shirika hili na watalamu wake wanafanya kazi nzuri sana, hili ni jambo zuri katika ujenzi wa taifa, na kulifanya taifa liweze kujitegemea, jambo linalo ombwa na kila mtu, hivyo kuwasaidia watu hawa ni muhimu sana, Atabatu Abbasiyya tukufu itaendelea kutoa msaada kwa viwanda kama hivi”.

Sayyid Ashiqar alipokelewa na mkuu wa shirika hilo, Ustadh Maitham Bahadeli, na alipewa maelezo ya kina kuhusu utendaji wa shirika hilo kutoka kwa wafanya kazi wa shirika, ambao walimweleza bidhaa wanazo zalisha kwa sasa na wanazo tarajia kuzalisha hapo baadae.

Mwishoni mwa ziara katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, alisifu utendaji mzuri wa wafanyakazi wa shirika hili na akawahimiza waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kutumikia taifa la Iraq na kulinda rasilimali za kilimo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: