Kituo cha faharasi na kupangilia taarifa katika Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya semina ya kuwajengea uwezo watalamu wake katika fani ya kuongea na kuathiri…

Maoni katika picha
Miongoni mwa muendelezo wa semina za kujenga uwezo zinazo changia kuongeza utalamu na kuboresha fikra, kituo cha faharasi na kupangilia taarifa chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake katika fani ya kuongea na kuadhiri wengine, kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, pia inasaidia kujifahamu mwenyewe na kufahamu utashi wa wengine.

Semina ilikua ya siku nne, na kila siku walisoma masaa manne, jumla ya washiriki walikua (16), lengo la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuzungumza na kutoa mihadhara katika mahafali ya kitaifa na kimataifa.

Ustadh Farasi Abdurazaaq Shimri aliye kua mkufunzi katika semina hii, amesema kua: “Tulikua na ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo cha faharasi kilicho chini ya maktaba katika kitengo cha habari na utamaduni, kwani kutokana na majukumu ya watumishi wanahitaji semina za kujengewa uwezo na kuangalia utendaji wa maktaba zingine pamoja na kukutana na wanafunzi wa vyuo vikuu, hivyo kulikua na haja kubwa ya kuwajengea uwezo wa kutoa mada na namna ya kuathiri watu wengine kwa kutumia njia bora zaidi”.

Akaendelea kusema: “Hakika kujiendeleza kielimu ni nguzo muhimu sana katika kila kazi inayo fanywa na taasisi yeyote, na kila mmoja kulingana na fani yake, semina hua ni masomo ya muda mfupi na yanafaida kubwa sana, huongeza kiwango cha utendaji, lengo kuu la kuwapa semina watumishi na watalamu mbalimbali hua ni kuondoa vikwazo wanavyo kutana navyo katika utekelezaji wa majukumu yao na kuongeza uwezo wao katika utendaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: