Marjaa dini mkuu katika khutuba ya ushindi: Walio itikia fatwa ya kujilinda hawakua na tamaa ya mali wala cheo. Hakika kupambana na ufisadi ni sawa na kupambana na ugaidi…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu katika khutuba ya ushindi ya Ijumaa iliyo pita, amesisitiza kuwajali walio itikia wito wa fatwa ya jihadi ya kujilinda, na kuacha kutumia uzalendo na kujitolea kwao kwa maslahi binafsi ya kisiasa jambo linalo pelekea kuvunja utukufu wa nia zao.

Katika kipengele cha mwisho cha khutuba yake amesisitiza kua wairaq wanaweza kushinda vita dhidi ya ufisadi –kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu- iwapo watawekewa mazingira mazuri ya kufanya hivyo, akiashiria umuhimu wa kupambana na ufisadi pamoja na mafisadi, na kwamba hatua inayo fuata inabidi iwe ni vita dhidi ya ufisadi wa mali na kiofisi kwa kufuata misingi ya katiba na sheria.

Sehemu ya khutuba iliyo zungumzia swala la kupambana na ufisadi inasema kua: “Hakika asilimia kubwa ya watu walioshiriki katika vita miaka ya hivi karibuni, hawakushiriki kwa ajili ya maslahi ya dunia yao au kupata cheo, waliingia vitani kwa ajili ya kuitikia mwito wa Marjaa wao na kutekeleza wajibu wa kitaifa na kidini, kilicho wasukuma ni mapenzi yao kwa taifa na wananchi, na kuhakikisha wanalinda heshima ya wairaq isivunjwe na magaidi ya Daesh, na kulinda maeneo matakatifu yasiharibiwe na magaidi, walikua na nia njema isiyo kua na tegemeo la kutafuta mali, wanastahiki heshima ya pekee kutoka kwa wananchi wote isiyo lingana na kikundi au chama chochote cha kisiasa, ni muhimu sana kulinda heshima yao bila kujaribu kutafuta umaarufu au kupata nafasi za kisiasa kupitia wao, kufanya hivyo ni kuwavunjia heshima na kulifanya jambo hili kua sawa na mambo mengine yaliyo pita na yakasahaulika kutokana na makosa yaliyo fanywa na watu hao”.

“Hakika kupambana na ufisadi ni hatua muhimu inayo paswa kuchukuliwa, lazima tupambane na ufisadi wa mali na kiofisi kwa nguvu zote, na sio zima moto au maigizo, hakika vita dhidi ya ufisadi –ambayo imechelewa kuanza- madhara yake hayana tofauti na vita dhidi ya ugaidi bali inawezekana ufisadi una madhara makubwa mno kuliko ugaidi, raia watukufu wa Iraq walio pigana vita dhidi ya magaidi –kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu- wanaweza kupigana vita dhidi ya ufisadi na kuishinda kama watawekewa mazingira mazuri ya kupambana vita hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: