Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chafanya hafla ya kusherehekea ushindi wa Iraq…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya hafla ya kusherehekea ushindi wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh kwa kukomboa ardhi yote kutoka kwa magaidi hao, ulio patikana kwa juhudi za raia wa Iraq, hafla hiyo imefanywa siku ya Alkhamisi ya tarehe (2 Rabiul-Thani 1439h) sawa na (21 Desemba 2017m), katika ukumbi wa Naqaba Mualimina Mkoani Karbala, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Karbala pamoja na wawakilishi wa Hashdi Sha’abi.

Baada ya kusomwa surat Fat-ha na kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Maitham Zaidi, ambaye alianza kwa kumsifu Marjaa dini mkuu na raia wa Iraq pamoja na jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi kwa juhudi zao zilizo leta ushindi huu mkubwa, pia aliwakumbuka mashahidi kwani wao hasa ndio walio sababisha ushindi huu kwa damu zao takatifu.

Akaongeza kusema kua: “Hakika Iraq imetoka katika vita kubwa ya kihistoria iliyo kua tishio baya mno, kila anaye litakia taifa hili mabaya aliishabikia vita hiyo, lakini raia wa Iraq wameweza kuondoa hatari hiyo na kumshinda adui aliye lenga kuvunja misingi ya ubinadamu, tamaduni na historia, na alikusudia kuharibu kila zuri hapa Iraq, kwa utukufu wa wito wa Marjaa dini mkuu wa fatwa ya jihadi ya kujilinda na kulinda taifa na maeneo matakatifu, fatwa hiyo ilikua mwongozo mkuu wa watu walio jitolea kupigana, watu wakatoka kwa wingi kwa ajili ya kutekeleza wito huo, miongoni mwao kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji pamoja na vikosi vingine vya Hashdi Sha’abi”.

Akaendelea kubainisha kua: “Kwa ajili ya kukumbuka jambo hili na kushukuru juhudi za raia wa Iraq kwa kuwashinda magaidi wa Daesh, na kwa ajili ya kuchangia katika kuhifadhi historia ya kikosi cha Abbasi (a.s) na mchango wao katika vita hiyo, tumeandaa ripoti itakayo kua inarushwa katika vyombo vya habari ikionyesha mapambano yao na namna walivyo jitolea katika vita hii tukufu”.

Baada ya ujumbe huo, kikosi cha Abbasi (a.s) kikapewa midani, iliyo tolewa na Ustadhi Ridhwa Kar’awi na kupokelewa na Shekh Maitham Zaidi.

Kisha likafanyika igizo lililo andaliwa na umoja wa waigizaji wa kiiraq na pewa jina la (Twende tukajenge taifa), lililo buniwa na Ahmadi Hatifu na kupangiliwa na As-adi Mishawi.

Igizo lenye muda wa dakika 40, lilifatiliwa kwa karibu sana na wahudhuriaji, igizo hilo linaonyesha kisa cha watu watano walio ishi katika mazingira halisi ya kipindi cha hivi karibuni, kuna kijana mkristo aliye poteza mpenzi wake katika mji wa Mosul na akaamua kupigana dhidi ya magaidi, na kijana mwingine alinusurika katika mauaji ya Spaika, anahadithia yaliyo mkuta, miongoni mwa kisa chake kuna namna alivyo saidiwa na mwanamke, na kuna kijana anaye taka kujiunga na Hashdi Sha’abi lakini ana tatizo toka miaka 12 ya nyuma, alipoteza vielelezo vyote vinavyo thibitisha kua yeye ni raia wa Iraq, kwa hiyo bado anajishauri aende au asiende, ili aende ni lazima apate idhini ya mama yake, na mtu mwingine ni Shahidi Mustwafa Adhari aliye uliwa na magaidi wa Daesh, kabla ya kuuawa kwake walimuweka alama katika mwili wake zenye ujumbe wa wazi, naye aliendelea kua na msimamo hakuogopa kufa hata kidogo, kwa hiyo waigizaji walionyesha mazingira hayo tofauti.

Mwisho wa hafla hiyo kikosi cha deraya cha Tisha katika jeshi la serikali kilicho kua kikipigana mara nyingi bega kwa bega na kikosi cha Abbasi (a.s) kikapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: