Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya semina ya kuwajengea uwezo katika mambo ya utawala marais wa vitengo vyake…

Dokta Taqi Abdiwani
Kwa lengo la kuongeza uwezo wa utendaji wa kiofisi na maswala ya kiutawala, Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa semina kwa marais wa vitengo vyake kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji wao, jambo ambalo linatarajiwa kua na matokeo mazuri katika utekelezaji wa majukumu yao, Ataba tukufu imekua ikitoa semina mara nyingi kwa watumishi wa vitengo mbalimbali pamoja na viongozi wao zinazo lenga kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

Semina hii inaendeshwa na kituo cha Alkafeel na kusimamiwa na dokta Taqi Abdiwani mkuu cha chuo kikuu cha Khalij katika mji mkuu wa Oman (Muscat), kwa mujibu wa maelezo yake, “Semina hii inalenga kuwajengea uwezo katika maswala ya uongozi wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ambao ni marais wa vitengo, na imeangazia mambo mawili:

Jambo la kwanza: Linahusu mpango mkakati na mpango kazi, vitu vinavyo elezea namna ya kuboresha utendaji wa watumishi na inasaidia kunadhimu (kupangilia) utendaji wa taasisi.

Jambo la pili: lina njia mbili, ya kwanza ni njia ya mafanikio ambayo inaitwa (Kaizen) inayo lenga kua na maendeleo endelevu, nao ni mfumo wa kisasa wa kijapani, unalenga kuleta mabadiliko bora yanayo tafsiriwa na maendeleo endelevu, mfumo huo unahusisha maendeleo ya kiuzalishaji, kiteknolojia na kiofisi, unaweza kuutumia kazini, nyumbani au ofisini kulingana na mazingira ya taasisi husika. Njia ya pili ni kupunguza watendaji na kuongeza uzalishaji katika sehemu yeyote.

Akamaliza kwa kusema: “Kwa hakika washiriki wametoa ushirikiano mkubwa sana na wana utayari mkubwa wa uwajibikaji na kuhisi majukumu ya kiofisi na kitaasisi katika kazi zao, tunatarajia watanufaika sana na semina hii na kua chachu ya kuongeza ufanisi katika huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa jamii”.

Mshauri wa kiuchumi katika kituo cha Alkafeel dokta Swafaa Mussawi amesema kua: “Hakika uongozi mkuu wa Ataba tukufu unaona kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wake hususan wale wanaofanya kazi katika ofisi kuu, kutokana na umuhimu huo; kituo cha Alkafeel kimeandaa semina hii inayo husu mpango mkakati na mpango kazi, kwa kuangalia aina ya (Kaizen) ambao ni mfumo wa kijapani, unao lenga kupunguza watendaji na kuongeza uzalishaji, na wakawasiliana na dokta Taqi Abdiwani kutoka Omani kwa ajili ya semina hii, fahamu kua semina hii nimiongoni mwa semina muhimu sana”.

Washiriki wamesisitiza umuhimu wa semina hii, wamesema ni njia ya kuelekea katika mafanikio, pia inasaidia kuongeza uwezo wa kiutendaji kwa mtu mmoja mmoja na kufahamu namna ya kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kwa njia rahisi pamoja na kupima mafanikio ya taasisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: