Miongoni mwa misafara ya kutoa misaada ya kibinadamu katika miji iliyo kombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, sehemu ya pili ya msafara ulio anzia mji wa Sanjaar katika mkoa wa Nainawa wa kutoa misaada ya kibinadamu, Atabatu Abbasiyya imeuelekeza msafara huo kuelekea katika mpaka wa Iraq na Sirya kwa ajili ya kwenda kugawa misaada kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi wanao linda mpaka huo, msafara huu ulianza sambamba na sherehe za kukombolewa kwa ardhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kamati ya maelekezo na misaada, wamekua mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kimkakati na chakula pamoja na vifaa vingine muhimu vinavyo hitajiwa na wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, walianza kufanya kazi hii toka kuanza kwa vita ya kukomboa ardhi ya Iraq baada ya fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda na hawajapumzika hadi sasa, daima walipatikana katika vikosi mbalimbali vya wapiganaji kuanzia vita ya kukomboa mji wa Jurfu-Nasri hadi mpakani.
Msafara wa kutoa misaada ni sehemu ya aina nyingi ya misafara inayo tumwa na kamati ya maelekezo na misaada ya kimkakati katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kutafuta ushindi wa vita na kusaidia mahitaji ya wapiganaji, ambapo hugawa chakula, mavazi ya kujikinga na baridi pamoja na mavazi ya kijeshi na majaketi ya mvua, vilevile hugawa vifaa vya kulalia na kujifunika na vinginevyo miongoni mwa vifaa muhimu kwa wapiganaji, wamesha gawa misaada kwa vituo vyote zaidi ya hamsini vya wanajeshi wanao linda mpaka wa Iraq na Sirya.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutuma misafara ya kutoa misaada ya chakula na vifaa kwa vikosi vyote vya wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, pia wameunda kamati maalumu kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi.