Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha nadwa kuhusu mradi wa mausua ya fatwa tukufu ya kujilinda…

Maoni katika picha
Kutokana na ushindi wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali, asubuhi ya Juma Tano (8 Rabiul-Thani 1439h) sawa na (27 Desemba 2017m) katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), kamati zilizo simamia misafara ya kutoa misaada kwa familia za wakimbizi zilifanya nadwa.

Nadwa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, halafu ukafuatia muhadhara wa kidini, ulio husu kumbukumbu ya kufariki kwa mtakasifu Zaharaa (a.s), muhadhara ulitolewa na Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawi, alielezea dhulma alizo fanyiwa Swidiqat Zaharaa (a.s) na yaliyo jiri kwake baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w).

Baada ya hapo Mheshimiwa Sayyid Leeth Mussawi rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akatoa sherehe ndefu kuhusu vitabu (mausua) ya fatwa tukufu ya kujilinda, alibainisha kua: “Baada ya kutolewa fatwa ya jihadi ya kujilinda na kuanzishwa Hashdi Sha’abi tukufu, inatakiwa kuwepo na udhibiti wa kila kilicho fanyika katika uwanja wa vita na namna wanajeshi wa serikali walivyo saidiwa, ndipo ikatujia fikra ya kuanzisha mausua (vitabu) vya fatwa tukufu ya kujilinda, kwa lengo la kuandika mambo hayo ili historia ihifadhi damu za mashahidi”.

Sayyid Leeth Mussawi akasema kua vitabu (mausua) viyo itakua na juzuu (24), kila juzu litakua na mada maalumu, kisha akaanza kuelezea mradi huu mkubwa:

  • Juzuu la kwanza: linahusu mambo ya kihistoria, linaelezea harakati za watu wenye imani kali za kibaguzi, na mashambulizi ya mawahabi katika mji wa Karbala, na utendaji wa vyombo vya habari baada ya mwaka 2013.
  • Juzuu la pili: Marjaa dini mkuu na misimamo yake ya kitaifa, na limegawanyika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza: Athari ya Marjaa dini mkuu katika kuilinda Iraq kufuatia fatwa ambayo ilianzisha harakati za mwaka (1920). Sehemu ya pili: Marjaa dini mkuu na msimamo wake katika upande wa kisiasa, kitaifa na kiarabu kuanzia mwaka (1921 – 2003). Sehemu ya tatu: Marjaa Sayyid Sistani na athari yake katika mambo ya kitaifa nchini Iraq baada ya mwaka (2003).
  • Juzuu la tatu: linaelezea harakati za kijeshi baada ya mwaka (2014) na linasehemu tatu. Sehemu ya kwanza: Inaelezea kutekwa miji, kuanzia kutekwa kwa mji wa Mosul na kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda na namna ilivyo itikiwa na raia. Sehemu ya pili: Imenukuu khutuba za Ijumaa zilizo elezea maswala ya kiusalama hapa Iraq kuanzia mwaka (2014 – 2017). Sehemu ya tatu: Inaelezea harakati za kijeshi na kukombolewa kwa miji iliyo tekwa.
  • Juzuu la nne: Linaelezea juhudi zilizo fanywa na hauza ya mji mtukufu wa Najafu, na lina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza: Inaelezea msaada wa kimkakati waliopewa vikosi vya jeshi. Sehemu ya pili: Inaelezea misaada ya vifaa na watu wa hauza walio uawa kishahidi.
  • Juzuu la tano: Linaelezea juhudi zilizo fanywa na Ataba tukufu za Iraq, za kusaidia askari kwa kuunda vikosi vya wapiganaji, na kutoa misaada ya kimkakati na kibinadamu pamoja na kusaidia katika sekta ya habari.
  • Juzuu la sita: Linaelezea juhudi za vyombo vya habari, misaada ya kibinadamu na vita za kukomboa miji, Na lina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza: Nafasi ya vyombo vya habari katika kutangaza fatwa tukufu kieneo na kimataifa. Sehemu ya pili: Umuhimu wa vyomba vya habari katika sekta ya misaada ya kibinadamu. Sehemu ya tatu: Umuhimu wa vyombo vya habari katika vita ya ukombozi.
  • Juzuu la saba: Linaelezea misaada ya kimkakati na kibinadamu kwa Hashdi Sha’abi, na lina sehemu mbili: Sehemu ya kwanza: Mawakibu (vikundi) vya Husseiniyya. Sehemu ya pili: Juhudi za taasisi na raia.
  • Juzuu la nane: Watu walio uawa kishahidi kutokana na fatwa tukufu.
  • Juzuu la tisa: Linaelezea Fatwa tukufu katika jicho la watafiti, lina sehemu tatu, Sehemu ya kwanza: Yaliyo andikwa zaidi na watafiti kuhusu fatwa. Sehemu ya pili: Makala zilizo sambazwa zaidi kipindi kilicho pita. Sehemu ya tatu: Yaliyo simuliwa kuhusu ujasiri wa wapiganaji.
  • Juzuu la kumi: Yaliyo andikwa kwa lugha zingine katika tafiti na Makala za kigeni.

Baada ya hapo kikaingia kipindi cha kutoa maoni na michango kutoka kwa wawakilishi wa Marajii na Mawakibu pamoja na taasisi zilizo toa misaada ya kimkakati walio kuja kutoka mikoa yote ya Iraq.

Kumbuka kua mradi huu ulio fanywa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kutunza taarifa zote muhimu na ulianza kutekelezwa zaidi ya mwaka na nusu ulio pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: