Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Hakika kilicho fanywa na shirika la Juud, kutengeneza bidhaa katika kipindi kigumu ni mafanikio…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ziara na matembezi anayo fanya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ya kuangalia viwanda na uzalishaji unao fanywa na vituo vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, safari hii ametembelea shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Juud na kuangalia utendaji na uzalishaji wake, pamoja na kuangalia matatizo au changamoto wanazo weza kukutana nazo, na kuzipatia utatuzi ufaao kwa maendeleo ya kiwanda hiki muhimu, kilicho onyesha mafanikio na kuweza kutoa bidhaa zenye ubora mkubwa unao zidi bidhaa zilizopo katika soko la Iraq, bidhaa za mbolea na vifaa, kimechangia kuirudisha Iraq katika nafasi ya viwanda ambayo ilikua imepotea kwa muda mrefu.

Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ambae alifuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), baada ya kutembelea sehemu za kiwanda hicho, na kusikiliza maelezo ya kina kutoka kwa meneja mkuu wa shirika Ustadh Maitham Bahadeli, alisisitiza “Umuhimu wa kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora mkubwa kwa kuzingatia mahitaji ya watumiaji wa kiiraq, hakika mafanikio yaliyo patikana wakati wa kipindi kigumu tulicho pitia kama taifa siku za nyuma, yanatokana na juhudi za watumishi”.

Na mwisho, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu akawasifu watumishi wa shirika hili kwa kazi nzuri wanayo fanya, akawaomba waongeze juhudi katika kuwatumikia wairaq na kulinda rasilimali za kilimo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: