Mu’ujamu (kitabu) cha maneno ya Qur’an mbele ya Ahlulbait (a.s), ni toleo jipya katika masomo ya Qur’an…

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa machapisho yake ni kitabu cha maneno ya Qur’an tukufu mbele ya Ahlulbait (a.s), nalo ni toleo muhimu katika masomo ya Qur’an, mtunzi ni Dokta Dhargham Karim Mussawi, chini ya usimamizi mkuu wa Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Halo, na kikahakikiwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, kitabu hiki ni miongoni mwa matoleo muhimu katika masomo ya Qur’an.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawaad Nasrawi amezungumza kuhusu swala hili kua: “Hakika maarifa ya Qur’an anayo hitaji sana mtafiti ni milango ya maneno ya Qur’an na kubainisha makusudio yake, hivyo ndio vitu vya msingi kwa mtafiti, kuna vitabu vizuri vya fani hii lakini ni vya zamani, miongoni mwa vitabu hivyo ni, kitabu cha maneno ya Qur’an tukufu kilicho andikwa na (Raaghibu Isfahani) na vingine vingi vilivyo andikwa katika fani hii lakini havikidhi haja, na wala haviendani na mazingira ya sasa, ulikua unahitajika uhuishaji katika sekta hii, ndipo kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha kikaamua kutoa kitabu hiki, limekua jambo jema na lenye manufaa makubwa katika kudhihirisha tafsiri ya Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kua kituo cha Maahadi ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha ni moja ya vituo hai katika Maahadi ya Qur’an tukufu, na tumesha tekeleza miradi mingi ya Qur’an tukufu inayo changia kueneza utamaduni na uwelewa wa Qur’an, miongoni mwa miradi hiyo ni kuchapisha msahafu rasmi ambao ni toleo la Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo hilo lilikua mafanikio makubwa katika sekta hiyo kwa sababu ndio msahafu wa kwanza kuchapishwa hapa Iraq, kabla ya hapo ilikua inachapishwa na taasisi za nje ya nchi, pia wana matolea mengi ya vitabu vya masomo ya Qur’an vinavyo lenga kutoa elimu na muongozo wa vizito viwili, pamoja na kufanya semina na nadwa mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: