Atabatu Abbasiyya tukufu yaupamba mji wa Karbala kwa mabango yanayo onyesha mwelekeo wa Kibla…

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi ya kiutamaduni inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuifanya jamii ipambike na tabia za Ahlulbait (a.s) na ifuate misingi ya muhanga wa Imamu Hussein (a.s), idara ya mabango katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi, chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wametekeleza mradi wa kuweka mabango yanayo onyesha mwelekeo wa Kibla katika barabara kuu za mkoa mtukufu wa Karbala.

Jopo la mafundi wa idara tajwa hapo juu kwa kushirikiana na kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameweka mabango (25) yanayo onyesha mwelekeo wa Kibla, kuanzia eneo la Iskaan hadi barabara ya Husseiniyya na barabara ya Maitham Tamaar.

Mradi huu ni miongoni mwa mipango iliyo wekwa na Ataba tukufu, ya kuwaelekeza watu wanaokuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku za kawaida au katika matukio maalumu yanayo hudhuriwa na mamilioni ya mazuwaru (watu), mabango hayo yana alama ya mshale ulio andikwa maneno yanayo julisha mwelekeo wa Kibla, na yamefungwa katika nguzo zilizopo katika barabara kuu, ili kuwawezesha watu wanao ingia katika mji wa Karbala kuelewa kwa urahisi mwelekeo wa Kibla na kutekeleza ibada ya swala kwa wakati.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: