Kugawa mialiko ya kushiriki katika shindano la kitaifa la fani ya kuhutubia.. na wakuu wa vitengo vya malezi wathibitisha kushiriki kwa wanafunzi wao na wasema ni jambo lenye mafanikio…

Maoni katika picha
Ofisi ya shughuli za kishule katika idara ya mahusiano na vyuo vikuu, chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kufanya maandalizi ya shindano la kitaifa la awamu ya tatu katika fani ya kuhutubia kwa wanafunzi wa shule za sekondari (upili), linalo tarajiwa kufanyika ndani ya mwezi Machi.

Imetolewa mialiko sambamba na masharti ya shindano kwa ofisi za malezi zilizopo katika mikoa ya kati na ya kusini, nazo zitasambaza mialiko hiyo katika shule mbalimbali, ili zichague wanafunzi watakao shiriki katika shindano hilo kwa kufuata vigezo na masharti yaliyo wekwa na kamati ya maandalizi, ambapo wanafunzi hao watapata nafasi ya kuandaa mada zao na kuzifanyia mazowezi, kwani zitashindanishwa chini ya jopo la majaji na zitachaguliwa mada tano za ushindi.

Maandalizi ya awamu hii yameanza mapema, kwa ajili ya kuzipa shule muda wa kutosha kuchagua washiriki, na kuifanya awamu ya tatu kua bora zaidi ya awamu mbili zilizo pita.

Kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi wa shindano hili, mada zitahusu mambo mawili makuu, ambayo ni: Kupenda nchi na kulisaidia jeshi la taifa na Hashdi Sha’abi, na ushindi walio pata dhidi ya magaidi wa Daesh kwa kufanikiwa kukomboa ardhi yote ya Iraq.

Wakuu wa vituo vya malezi katika mikoa ya kati na kusini wamethibitisha kushiriki kwa wanafunzi wao katika shindano hili, na wakasema kua litakua la aina yake na lenye mafanikio, linatoa hamasa ya kushindana baina ya wanafunzi, na litatengeneza makhatibu bora hapo baadae, na wakaomba kwa waandalizi wa shindano hili wahakikishe wanawafikia wanafunzi wa ngazi zingine pia.

Kumbuka kua wanafunzi walio shiriki katika shindano hili mwaka jana walikua (45), kutoka katika ofisi kuu za malezi za (Karbala tukufu, Najafu, na Bagdadi, nafasi ya kwanza na ya pili zilishikwa na wanafunzi kutoka Bagdadi, na nafasi ya tatu ikashikwa na Muthanna, Waasit, Basra, Baabil, Dhiqaar na Qadisiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: