Kwa picha: Shamba boy wa Alkafeel waweka mauwa katika mlango wa Kibla wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Watalamu wa shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka mauwa ya aina mbalimbali katika mlango wa Kibla, kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mauwa hayo yamepangwa vizuri kiasi ambacho yanawafurahisha watu wanaokuja kutembelea sehemu hii takatifu, bila shaka mauwa haya yamependezesha eneo hili tukufu.

Hii ni sehemu ya kazi za Shamba boy wa Alkafeel katika kipindi chote cha mwaka, pia wamepamba maeneo mawili muhimu, ambayo ni; upande wa nje wa mlango mkuu wa Kibla, pamoja na upande wa ndani, sehemu zote mbili zimepambwa kwa mauwa ya mbalimbali.

Kwa upande mwingine; kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbaisyya tukufu, kimefungua sehemu nyingine ya kuingilia katika mlango ya Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyopo upande wa kushoto, ambayo hapo awali ilikua inatumika kwa ajili ya kukaa na kulala mazuwaru, hii ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuingiza watu wengi zaidi, na yamefunguliwa madirisha ya kutunza vifaa (amanaat) katika eneo hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: