Miongoni mwa machapisho ya turathi za Qur’an: Kituo cha turathi za Karbala chatoa kitabu cha maarifa ya Qur’an kutokana na maandishi ya Sayyid Hibat Dini Alhusseiniyyu Shaharistaniyyu…

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kinaendelea kutoa vitabu vya turathi, kimeandaa milango na faharasi za turathi chini ya usimamizi wa kamati ya wataalamu wa sekta hiyo, miongoni mwa vitabu vya turathi walivyo toa; ni kitabu cha turathi za Qur’an, hivi karibuni wametoa kitabu cha (Maarifa ya Qur’an tukufu katika maandishi ya Sayyid Hibat Dini Alhusseiniyyu Shiraziyyu).

Kitabu kina kurasa 547 na kina milango mikuu miwili, mlango wa kwanza una sehemu nne kama ifuatavyo:

  • Sehemu ya kwanza: Kinga ya kutobadilishwa kwa Qur’an – Ina mada tatu.
  • Sehemu ya pili: Ifutayo na ifutwayo (Nasikhu na Mansukhu) ndani ya Qur’an tukufu – Ina mada tatu.
  • Sehemu ya tatu: Muhkamu na Mutashabiha ndani ya Qur’an tukufu – Ina mada tatu.
  • Sehemu ya nne: Maajabu ya balagha ndani ya Qur’an tukufu – ina mada tatu.

Mlango wa pili una sehemu nne pia, kama ifuatavyo:

  • Sehemu ya kwanza: Kinga ya kutobadilishwa kwa Qur’an – Ina mada mbili.
  • Sehemu ya pili: Ifutayo na ifutwayo (Nasikhu na Mansukhu) ndani ya Qur’an tukufu – Ina mada sita.
  • Sehemu ya tatu: Muhkamu na Mutashabiha ndani ya Qur’an tukufu – Ina mada sita.
  • Sehemu ya nne: Maajabu ya balagha ndani ya Qur’an tukufu – Ina mada nne.

Kumbuka kua kitabu hiki kimetokana na juhudi za kituo cha turathi za Karbala, kwa kutilia umuhimu masomo yaliyo andikwa na wanachuoni wa mji huu mtukufu, hususan masomo ya Qur’an ambayo ndio yanayo kusudiwa zaidi na kituo hiki, na kuandaa (mtiririko wa turathi za Qur’an), nacho ni sehemu ya mtiririko wa vitabu vinavyo tolewa na kituo hiki, na kina ongeza orodha ya vitabu vinavyo elezea turathi za mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: