Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amerudia kuonyesha imani yake kwa watalamu wa chuo kikuu cha Ameed, kua wana uwezo mkubwa wa kuleta mafanikio ya kielimu…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameonyesha imani kubwa kwa watalamu wa chuo kikuu cha Ameed, akasema kua wanauwezo mkubwa wa kuleta maendeleo na kukiweka chuo katika nafasi ya kutoa ushindani kwa vyuo vingine vya ndani na nje ya Iraq.

Aliyasema hayo katika mkutano wa kielimu ulio andaliwa na chuo kikuu cha Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wenye kauli mbiu isemayo (Mpango wa Alkafeel wa kuinua kiwango cha elimu ya vyuo vikuu), mkutano huo pia ulihutubiwa na dokta Shaamil Muhsin Haadi, mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya huko Marekani na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ocoland.

Sayyid Swafi amesema kua “Wakufunzi wa chuo kikuu cha Ameed wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanafunzi wanao hitimu masomo katika chuo hiki wanakua na kiwango kikubwa cha elimu, kitakacho wawezesha kutoa ushindani kwa vyuo vikuu vya kitaifa na kimataifa, na sisi tuna imani kubwa na wakufunzi wote wa chuo kikuu cha Ameed, wanauwezo mkubwa wa kutoa ushindani kwa vyuo vikuu vya Iraq, na kukiweka katika orodha ya vyuo bora kielimu”.

Mkutano huu wa kwanza wa aina yake kufanywa na chuo kikuu cha Ameed, unao husu namna ya kuboresha kiwango cha elimu katika vyuo vikuu. Mhadhiri alitoa nasaha kwa wakufunzi wa chuo kikuu cha Ameed na wanafunzi, na akasema kua chuo kina kiwango kizuri cha elimu hapa Iraq, na kinafuata selebasi ya vyuo vikuu vya ulaya, ambayo ni bora zaidi, inamuwezesha mwanafunzi kuelewa masomo vizuri na kwa urahisi.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqari, pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, pamoja na rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Dida na mkuu wa taaluma Dokta Jaasim Ibrahimi, pamoja na rais wa chuo kikuu Dokta Jaasim Marzuk, pamoja na wahadhiri wengine wengi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: