Ofisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya maonyesho ya vitu nadra na vya kihistoria katika kituo cha utamaduni huko Bagdadi…

Maoni katika picha
Idara ya maktaba na Daru Makhtutwaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni cha Bagdadi wanafanya maonyesho ya vifaa kale na nakala kale, ambapo kimeshiriki kituo cha upigaji picha wa nakala kale na utengenezaji wa faharasi zake, pamoja na idara ya uandishi na masomo sambamba na kituo cha uhuishaji wa turathi katika idara ya ofisi.

Maonyesho haya yamefanywa katika ukumbi wa (Muhammad Ghina) ndani ya kituo cha utamaduni cha Bagdad, vitu vinavyo onyeshwa vimegawanywa sehemu tatu kutokana na aina ya vitu hivyo, kituo cha upigaji picha za nakala kale na faharasi, kinaonyesha picha za vifaa kale na nakala kale, ikiwa ni pamoja na picha za msahafu mtukufu za tangu karne ya kwanza hijiriyya hadi karne ya kumi na tatu, pia wanaonyesha picha za zamani, zinazo onyesha zama mbalimbali katika historia ya uislamu, ukiwemo ubao wa picha ya Sharifu Idrisa ya tangu karne ya sita hijiriyya, inayo onyesha ramani ya zamani zaidi iliyo chorwa katika zama hizo, na kitu kingine kilicho onyeshwa ni maji ya tangu zama za utawala wa Othmaniyya, yaliyo tokana na bishara ya watu wa Najafu kwa wanachuoni wa dini wa kipindi hicho yaliyo toka na kukatika, hali kadhalika kulikua na machapisho ya kituo cha faharasi na nakala kale pamoja na msahafu wa mtafiti ibun Bawaab.

Idara ya uandishi na masomo imeonyesha aina mbalimbali za machapisho yake, ikiwemo majarida kuhusu historia ya mwezi wa bani Hashim (a.s) na kitabu cha (Abulfadhil Abbasi katika lugha na mashairi ya kiarabu) pamoja na vitabu vingine vinavyo muhusu Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kituo cha uhuishaji wa turathi nacho kilikua na utajiri wa vitu, kimeonyesha vitu mbalimbali miongoni mwa kazi zake, ikiwa ni pamoja na kitabu cha (Aqrabu Majazaatu) na (Jarida la Khazaanah) na vitabu vingine vinavyo husu utafiti na uhakiki wa nakala kale, pamoja na kuonyesha orodha ya uhakiki walio fanya.

Vitu vilivyo onyeshwa vinafika 16 ambavyo histotia yake inaanzia karne ya kwanza hijiriyya hadi karne ya kumi na tatu, na jumla ya vitabu vilivyo oneshwa ni 70, miongoni mwa vitabu hivyo kuna vilivyo fanyiwa uhakiki na vingine vimeandikwa, pamoja na kuonyesha mihuri ya maktaba za Iraq na za nchi zingine za kiarabu na kiajemi.

Maonyesho haya yamepata sifa kubwa kutoka kwa wadau, na yamekua na mwitikio mkubwa wa vyombo vya habari, vilevile ni fursa kubwa ya kufahamu mambo ya kale.

Kumbuka kua maonyesho haya ni miongoni mwa utaratibu ulio pangwa na ofisi ya Daru Maktutwaat ya Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kubainisha na kuonyesha vifaa kale vilivyopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzitunza, pamoja na kukuza uhusiano kati ya Ataba na taasisi zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: