Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya warsha kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo cha kitaifa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kusaidiana na kushirikiana baina ya Atabatu Abbasiyya na kituo cha mafunzo cha taifa chini ya wizara ya kazi na bima za kijamii Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa warsha ya mafundi wa kutengeneza magari ya aina mbalimbali pamoja na ufundi chuma, katika ukumbi wa kituo cha kitaifa, kwa watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, warsha hii inafanyika chini ya makubaliano yaliyo fikiwa hapo awali, kwa ajili ya kuongeza ujuzi na uzowefu wa kutengeneza magari ili kuweza kufikia malengo kwa ufanisi mkubwa.

Warsha hii itaendelea kwa muda wa siku kumi mfululizo, kila siku itakua na saa (6) za mafunzo, jumla ya washiriki kutoka kitengo cha usimamizi wa kihandisi wako (12), katika warsha hii wanafundishwa namna ya kutambua Leham za kisasa na njia za kukata za kisasa, leham za bomba za chuma, na kuongeza uwezo wa Leham pamoja na kutambua aina za Leham, hali kadhalika wamefundishwa kutengeneza magari madogo na makubwa na kutafuta mahala penye ubovu kwa kutumia vifaa vya kisasa, pamoja na kufungua Injini na gia box.

Kumbuka kua kituo cha mafunzo cha kitaifa kimesha fanya semina nyingi za kuwafundisha watumishi wa Ataba tukufu, na ushirikiano bado unaendelea baina ya pande mbili hadi watakapo kamilisha mafunzo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: