Kati ya anuani 1000: Atabatu Abbasiyya tukufu yapata tunzo tano katika shindano la kitabu cha hauza, na maktaba yake kuonekana ni kituo bora cha usambazaji…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu itapewa tunzo tano katika shindano la mwaka wa kumi na tisa la kitabu cha hauza lililo pangwa kufanyika mwezi saba Jamadal-Ula 1439h, sawa na (25 Januari 2018m) katika mji mtukufu wa Qum huko Iran, walitoa taarifa kwa watu walio faulu na kuwataka wahudhurie kongamano hilo kwa ajili ya kupewa zawadi (tunzo).

Zawadi (tunzo) hizo zitaenda kwa vitabu vitano vifuatavyo:

  • - (Mausua ya Alamah Urdibadi) kilicho andikwa na Sayyid Mahdi Shirazi, na kuchapishwa na kituo cha kuhuisha turathi katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, kimepata tunzo kwa kua kitabu bora kilicho hakikiwa.
  • - (Irabu za Nahju balagha) kilicho andikwa na Ustadh Muhammad Jalil Abbasi Hasanawi, na kuchapishwa na idara ya masomo na usambazaji katika kitengo cha habari na utamaduni, kimepata tunzo ya kua kitabu bora.
  • - (Muhtasar Maraasimul-Alawiyyah) cha (mhakiki Hilly) na kilihakikiwa na (Ahmadi Ali Majidi Hilly) kikachapishwa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kimetata nafasi ya pili.
  • - (Msahafu mtukufu unao nasibishwa na Ali bun Hilali Al-Bagdadi anaye anajulikana kama Ibun Bawaab) kilicho hakikiwa na Ustadh Ali Swafaar na kuchapishwa na kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepata nafasi ya pili.
  • - (Muhtasar wa habari mashuhuri kuhusu maimamu kumi na mbili) kilicho hakikiwa na Sayyid Alaa Mussawi na kuchapishwa na kituo cha kuhuisha turathi katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepata nafasi ya pili.

Hakika vitabu hivyo vimeshindanishwa na aina 1000 ya vitabu vilivyo shiriki shindano hilo, na vimepasishwa na jopo la majaji mahiri.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa wasimamizi wa kongamano hilo zinasema kua, Daru Makhtutwaat iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepata nafasi ya kua kituo bora cha usambazaji katika shindano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: