Darasa mjadala (nadwa) za Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo zaendelea kupata mwitikio mkubwa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba za Qur’an zilizo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya umoja wa harakati kuhusu Qur’an katika idara ya mahusiano na vyuo vikuu, ni ratiba ya darasa mjadala (nadwa) kwa wanafunzi wa vyuo, zinazo endeshwa chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, ratiba hii inamwitikio mkubwa, jambo linalo pelekea wasimamizi wake kufikiria kupanua wigo wa ratiba, na kufikia vyuo vingine, kwa kupanga muda na sehemu bila kuathiri vipindi vya masomo yao, kwa upande mwingine, tumeongeza baadhi ya mambo katika ratiba hii, yanayo endana na akili za vijana pamoja na mahitaji yao ya nyumbani na chuoni.

Kamati inayo simamia ratiba, imeuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: Hakika wanafunzi wanapenda kusoma sheria zinazo tegemea dalili za Qur’an bila kua na ta’asub. Wakaongeza kusema kua: tumepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa wanafuni katika nadwa hizi na wamepanga muda katika ratiba zao za kila siku kwa ajili ya kushiriki nadwa hizi.

Fahamu kua nadwa hizi husimamiwa na mashekh watukufu ambao huteuliwa na Atabatu Abbasiyya na kuwekewa utaratibu wa kuongea na akili za wanafunzi kwa kuzingatia uwezo wa uwelewa wao tena kwa kutumia njia nyepesi na rahisi kueleweka, huchaguliwa mada maalumu na hupewa mtoa mada ambaye huwajibika kuiwasilisha na kuisherehesha sambamba na kutoa ushahidi wa Qur’an na hadithi za maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), baada ya hapo hufunguliwa mlango wa majadiliano, maswali na maoni kutoka kwa wanafunzi, ambapo mwanafunzi huruhusiwa kuuliza swali au kutoa maoni yake kuhusu jambo fulani moja kwa moja kwa mtoa mada, au kwa kutumia njia ya kuandika katika karatasi na mtoa mada huzikusanya na kujibu moja kwa moja kilicho ulizwa katika karatasi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: