Kitengo cha Mawakibu na maashimisho ya Husseiniyya chatoa zawadi kwa viongozi wa kijeshi katika mkoa wa Diwaniyya…

Maoni katika picha
Kama sehemu ya kuonyesha kujali juhudi kubwa walizo fanya katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya Immamu Hussein (a.s), na utendaji wao mtukufu walio onyesha kwa ajili ya kuhakikisha amani na usalama, kitengo cha Mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimefanya hafla ya kuwapa zawadi (kuwakirim) viongozi wa jeshi katika mkoa wa Diwaniyya.

Hafla hiyo ilikua na kauli mbiu isemayo: (Nyie ndio mnaohami taifa, kwa kuwepo kwenu amani na usalama vinapatikana), imefanyika kwa kushirikiana na wawakilishi wa Mawakibu ndani ya ukumbi wa Husseiniyya ya Dagharah na kuhudhuriwa na viongozi wa dini na makabila pamoja na watu wa usalama wakiongozwa na kamanda wa mkoa Farqad Isawi, na ugeni ulio wakilisha Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) wakiongozwa na rais wa kitengo cha Mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya bwana Riyadh Ni’mat Salmaan, ambae alizungumza katika hafla hii, alitoa shukrani nyingi kwa kila aliye changia kuleta amani katika mkoa wa Diwaniyya, mkoa ambao hupokea mamilioni ya mazuwaru kila mwaka, hususan katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein, mkoa huu haukushuhudia uvunjifu mkubwa wa amani kiasi cha kuwadhuru mazuwaru, zawadi hizi tunazo toa ni kuonyesha kua Ataba mbili tukufu na kitengo cha Mawakibu tunatambua na kuthamini kazi nzuri ya kuwalinda na kuhakikisha usalama wa mazuwaru. Kupitia wawakilishi wa mawakibu tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunadumisha amani na utulivu kwa wakazi wa Diwaniyya au kwa mtu anaye kwenda kufanya ziara huko Karbala.

Hafla ilipambwa na Kaswida za kimashairi na ikahitimishwa kwa kugawa zawadi na vyeti kwa viongozi wa jeshi waliobainika kutoa mchango mkubwa kwa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ambapo zawadi hizo zitawaathiri kinafsi na kuwajengea ari ya kuongeza juhudi katika kulinda taifa.

Kumbuka kua kitengo cha Mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya hufanya program mbalimbali kila wakati ndani ya kipindi cha mwaka mzima ndani na nje ya mkoa wa Karbala, hufanya makongamano, nadwa, maonyesho pamoja na kuadhimisha tarehe za kuzaliwa au kufariki kwa maimamu wa Ahlulbait (a.s) sambamba na kutekeleza majukumu yao ya msingi, na hafla hii ni sehemu ya shughuli zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: