Baada ya kufaulu kozi yake ya kwanza: Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya khutuba za wanawake yaanza kusajili wanafunzi wa awamu ya pili…

Maoni katika picha
Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya khutuba za wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza kusajili wanafunzi wa awamu ya pili iliyo pewa jina la Albatuli, watakao fundishwa mbinu za kutoa khutuba (muhadhara), kozi hii ni sehemu ya kukamilisha kozi ya kwanza iliyo pata mafanikio makubwa yaliyo changia kukuza uwezo wa wazungumzaji na kutengeneza kizazi kipya cha wahadhiri wenye kutumia njia za kisasa, hii ndio kazi ya Maahadi katika selebasi yake ya ufundishaji au katika kozo zake, ikiwa ni pamoja na kozi hii.

Kozi ni ya mwaka mmoja na nusu, siku mbili kila wiki (Juma Mosi na Juma Pili) na husomeshwa mada za:

  • - Masomo ya Fiqhi.
  • - Masomo ya Aqida.
  • - Mbinu za utoaji wa Khutuba (Muhadhara).
  • - Qur’an na Maarifa ya Qur’an.

Tambua kua usajili unaendelea katika Maahadi ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa maelezo zaidi piga namba zifuatazo: (07602334055 au 07810645244).

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa Maahadi hii; ni kuboresha tablighi upande wa wanawake, kutokana na umuhimu wao mkubwa hasa katika kipindi cha maombolezo, na kuhakikisha wanapanua wigo wao katika ufikishaji wa maswala ya Imamu Hussein tena kwa njia nyepesi na yenye kueleweka zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: