Hospitali ya rufaa Alkafeel yatangaza kufaulu kwa upasuaji wa kwanza wa kupandikiza figo…

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa kiiraq wanaofanya kazi katika hospitali ya rufaa Alkafeel, ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wametangaza kufaulu kwa upasuaji wa kwanza wa kupandikiza figo ambayo alijitolea kijana mwenye umri wa miaka thelathini kumpa ndugu yake, upasuaji huo umefanywa na daktari muiraq kwa kushirikiana na jopo la madaktari bingwa.

Mshauri mkuu wa maradhi ya figo katika hospitali hii, Dokta Riyadh Swaaigh amesema kua: “Hakika leo jopo la madaktari limefaulu kufanya upasuaji kwa mara ya kwanza wa kupandikiza figo kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini na tatu, ambaye amepewa figo na ndugu yake mwenye umri wa miaka thelathini wote wakazi wa mji mtukufu wa Karbala, jopo la madaktari walio fanya upasuaji huo liliongozwa na daktari bingwa raia wa Iraq aliye kua Marekani Dokta As’ad Abdu-Aun chini ya usimamizi wetu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika upasuaji huu ni wakwanza kufanywa na hospitali ya rufaa Alkafeel, ulifanyiwa maandalizi ya kutosha, tulikusanya vifaa vyote vinavyo hitajika katika upasuaji, hali ya mgonjwa na ndugu yake aliye jitolea figo wanaendelea vizuri, na tayali wamesha tolewa katika chumba cha hatari baada ya saa 24 toka kufanyiwa upasuaji, tunatarajia kumruhusu aliye jitolea figo, na nimatumaini yetu ataungana na ndugu yake aliye pandikizwa figo baada ya siku chache”.

Akasema kua: “Kuna maombi mengine ya mgonjwa anaye hitaji kupandikizwa figo mwenye umri wa miaka 23 ambaye mzazi wake mwenye umri wa miaka hamsini ndiye atakaye jitolea moja ya figo zake, na kuna mgonjwa mwingine mwenye umri wa miaka hamsini ambaye mwanaye mwenye umri wa miaka thelathini ndiye atakaye jitolea moja ya figo zake”.

Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel, ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesha fanya mamia ya upasuaji wa aina mbalimbali, na asilimia kubwa ulikua wenye mafanikio, mafanikio hayo yanatokana na nyenzo mbili kuu: kwanza uwezo wa madaktari wa kiiraq na wa kigeni wanao fanya kazi katika hospitali hii, pili uwepo wa vifaa tiba bora na vya kisasa, pamoja na baraka za mwenye jina la hospitali hii ya Alkafeel ambaye ni Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali unaweza kuangalia mtandao wa hospitali ambao ni: www.kh.iq au piga simu namba: (07602344444 au 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: