Mawakibu za maombolezo ya Fatwimiyya zaingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoa taazia katika kumbukumbu ya shahada ya Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Kama ada yao katika siku hizi za huzuni ambazo zinaumiza moyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wa nyumbani kwake (a.s), siku za kukumbuka shahada ya mtoto wa Mtume (s.a.w.w) Swidiqatu Kubra bibi Fatuma Zaharaa (a.s), mawakibu za kuomboleza msiba wa Fatwimiyya zinamiminika kuhuisha tukio hili, wakitekeleza kauli ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu), wakiangazia namna alivyo jitolea mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Zaharaa (a.s) na kubainisha namna alivyo dhulumiwa, pamoja na kuhimiza kushikamana na mafundisho ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika mawakibu za kuomboleza huanza kuwasili katika kipindi hiki cha huzuni za Fatwimiyya au kwa jina lingine (Muharam mdogo) kabla ya siku chache za kumbukumbu ya shahada ambayo inasadifu mwezi kumi na tatu Jamadal Aakhar na huendelea hadi siku za riwaya ya tatu, na huongezeka zaidi katika siku za Ijumaa, malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hufikiwa na mawakibu nyingi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, haya ndio maombolezo yaliyo zoweleka tangu zamani, watumishi wa kitengo chetu hunadhimu matembezi yao, ambapo huingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia mlango wa Kibla na baada ya kutoa taazia zao huelekea katika malalo ya Abu Abdilahi Hussein (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, watu wanaokuja kufanya ziara pia hushiriki katika mawakibu za maombolezo”.

Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kila kona ya dunia wanakumbuka tukio hili la kuuawa kishahidi kwa mtoto wa Mtume bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti zinazo elezea tarehe ya kifo chake (a.s), zote hizo zinathibitisha namna alivyo dhulumiwa na mitihani aliyopata, hadi akamuhusia mme wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche kaburi lake na ahakikishe jeneza lake halishuhudiwi na yeyote miongoni mwa wale walio mdhulumu na kuchukua haki yake, kwa mujibu wa riwaya, alifariki akiwa na umri wa miaka kumi na nane.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: