Ujumbe kutoka katika makumbusho ya Alkafeel watembelea makumbusho ya kihistoria katika mji mkuu wa Bagdad na waangalia njia bora zaidi ya maonyesho katika makumbusho…

Maoni katika picha
Katika kujenga uhusiano na ushirikiano pamoja na kubadilishana uzowefu, ujumbe kutoka katika makumbusho ya Alkafeel chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea makumbusho ya kihistoria katika mji mkuu wa Bagdad, wakatembea katika korido za makumbusho hayo na kuangalia mbinu za kisasa za maonyesho ya makumbusho pamoja na kuangalia vifaa kale nadra vilivyopo katika makumbusho hiyo.

Wakati wakizunguka katika korido za makumbusho Dokta Aqiil Zubeidi mbobezi wa elimu ya Jiolojia, aliye kua mwenyeji wa wageni hao, alikua anatoa maelezo ya kina kuhusu vifaa vilivyomo katika makumbusho na namna ya utunzwaji wake.

Rais wa makumbusho ya Alkafeel Ustadh Swadiq Laazim Zaidi, aliye kua kiongozi wa ujumbe huo, alibainisha kua; wamefanya ziara hii kutokana na wito walio pata kutoka katika makumbusho hiyo ya kihistoria, akasema: “Tumetembelea makumbusho hii na tumeona vifaa vilivyopo ndani yake, hasa aina mbalimbali za mawe na vifaa vya baharini, ambavyo pia vifaa vya aina hii vipo kwa wingi katika makumbusho ya Alkafeel, tumejadiliana kuhusu namna ya kusaidiana na kushirikiana kwa kubadilishana uzowefu na kuongeza ujuzi wa utunzaji wa mawe na vifaa vinavyo tokana na bahari”.

Fahamu kua ofisi ya makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya ziara kama hizi kila baada ya muda, kwa ajili ya kukutana na watafiti wa kisekula walio bobea katika sekta ya makumbusho kwa ajili ya kunufaika nao na kufungua milango ya ushirikiano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: