Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya vitabu vya watoto ya kimataifa awamu ya tatu katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu…

Maoni katika picha
Idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inashiriki katika maonyesho ya vitabu vya watoto ya kimataifa awamu ya tatu, yanayo simamiwa na kitengo cha malezi na makuzi ya watoto cha Atabatu Husseiniyya tukufu katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo (Tusome pamoja) kuanzia tarehe 10-17/02/2018m.

Maonyesho yalifunguliwa jioni ya Juma Mosi (23 Jamadal-Awwal 1439h) sawa na (10/02/2018m) kwa kushiriki nchi nne ambazo ni: (Iraq, Lebanon, Kuwait na Iran) kukiwa na jumla ya vituo ishirini na aina za vitabu zaidi ya (1000) vikiwemo vya utamaduni, dini, Sayansi na kila jambo linalo husu watoto, tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limeshiriki likiwa na zaidi ya aina arubaini ya vitabu.

Ustadh Sarmad Salim Hassan kiongozi wa idara ya watoto na makuzi, ameuambia mtandao wa kimataifa wa Alkafeel kua: “Maonyesho ya kimataifa ya vitabu vya watoto yanayo fanyika Karbala, ni nafasi muhimu ya kuangazia vitabu vya watoto na kuvifikisha katika mikono ya watoto wa Iraq yetu kipenzi, Mwenyezi Mungu awabariki wanao simamia mradi huu muhimu”.

Akaongeza kusema kua: “Mwaka huu tumeshiriki tukiwa na aina mbalimbali za vitabu vya watoto kuanzia (Riyadh Walaa) ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) hadi (Raihana utur) na kuvifikisha kwa watoto wetu kutoka nchi zote, na vinazidi aina arubaini, vikiwa na rangi tofauti, kila rangi inamaanisha kitu fulani, kuna vitabu vya (visa, picha, mashairi, sayansi, utamaduni, visa vya mitume na historia za watu wa nyumba ya Mtume (a.s), ili kuifanya malalo ya Imamu Hussein (a.s) kua sawa na taa linalo angazia njia ya mapenzi na kuweka amani na utulivu katika nyoyo za watoto wetu vipenzi”.

Ustadh Sarmad akaendelea kufafanua kuhusu ushiriki huu na aina ya vitabu wanavyo onyesha kwa kusema kua: “Kuna jarida la kila mwezi linalo tolewa na idara, ambalo ni (Riyahain) linahusu watoto wenye umri kati ya miaka (5 – 12), na kuna jarida la (Haidara) linalo husu vijana wa umri wa miaka (13 – 17), majarida hayo yamejaa mafundisho mbalimbali yanayo lenga kumfundisha maadili mazuri mtoto”.

Akaongeza kusema kua: “Machapisho ya idara ya watoto na makuzi hayapo katika lugha ya kiarabu peke yake, bali yametafsiriwa katika lugha za Kiengereza, Kituruki, Kifarsi na Kikurdi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: