Kukamilisha ratiba ya Skaut (Rabiu Maarifa ya pili): jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yafunga hema za program ya Reihanatu Rasuul kwa makundi mawili…

Maoni katika picha
Kukamilisha ratiba ya Skaut (Rabiu Maarifa ya pili) imeanza program ya hema za (Reihanatu Rasuul –s.a.w.w-) kwa makundi mawili, na itadumu siku nne, kuanzia 11 – 14 Februari 2018.

zimeandaliwa ratiba tofauti za makundi hayo mawili, kutokana na umri wa washiriki katika kila kundi, ratiba hizo zinasimamiwa na jopo la watalam na zinalenga mambo yafuatayo:

  • 1- Kuwaweka karibu na maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) pamoja na wafuasi wa mafundisho yao.
  • 2- Kujenga uzalendo kwa washiriki kupitia mihadhara maalum.
  • 3- Kujenga moyo ya umoja na kujitenga na vikundi.
  • 4- Kuwafundisha umihimu wa kujitegemea na kuto tegemea watu wengine kupitia mafunzo mbalimbali ya Skaut.
  • 5- Kujenga uwelewa kwa vijana kuhusu changamoto zinazo wazunguka ikiwa ni pamoja na upotoshaji wa baadhi ya vyombo vya habari.
  • 6- Kuongeza maarifa katika maswala ya kimaendeleo na kutambua vipaji vyao.
  • 7- Pamoja na yote tuliyo sema, hema hizi ni fursa ya mapumziko na kubadilisha mazingira waliyo kua wanaishi wanafunzi katika kipindi cha mitihani.

Pembezoni mwa ratiba hiyo, tulipokea ugeni wa Skaut kutoka katika jumuiya ya Skaut ya Sayyid Shuhabaa (a.s) kutoka katika mkoa wa Baabil, jopo la wana Skaut walio jiunga na jopo la Skaut ya Alkafeel, hema hizi ni za aina yake kwa kupokea jopo la wanaskaut kutoka mkoa mwingine, idadi yao jumla pamoja na wageni imefika wanachama wa Skaut 250.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: