Idara ya ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla ya kutoa zawadi kwa washiriki wa ratiba ya marafiki wa maktaba…

Maoni katika picha
Katika kumaliza awamu ya nne ya program ya marafiki wa maktaba, idara ya ofisi ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuwazawadia washiriki wa ratiba ya marafiki wa maktaba iliyo fanyika mwaka huu chini ya kauli mbiu isemayo (nyuma ya kila kitabu kuna fikra, zao la kila fikra zi hatua ya kwenda mbele).

Hafla imepata mwitikio mkubwa wa wanawake maarufu wa Karbala wanao julikana kwa juhudi zao za kushiriki katika mambo ya kielimu na kitamaduni ili kujenga jamii bora na madhubuti, hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaibwa wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na ukafuatia ujumbe wa kiongozi wa ofisi ya wanawake ambaye alisema kua: “Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kinafanya kila kiwezalo katika kuhakikisha inaboresha sekta ya malezi ambayo imejikita katika swala la dini, utamaduni na elimu ya sekula, ili kuhakikisha tunafika katika lengo la kuimarisha imani na elimu”.

Akaongeza kusema kua: “Natoa wito kwa wakina mama wote wawahimize watoto wao wa kiume na wakike washikamane na elimu na wanufaike na vitabu, ili safina yetu ijayo itembee kwa kufuata ratiba mpya na maoni mapya pamoja na fikra zitakazo saidia kujenga taifa na kukamilisha kazi waliyo ianza mashahidi”.

Baada ya hapo ikaonyeshwa filamu inayo elezea harakati za ofisi ya wanawake katika swala la elimu, iliyo tengenezwa na ofisi ya wanawake.

Kisha ukafuata muhadhara usemao (mapitio ya akili katika maneno) uliokua na mada mbili, mada ya kwanza ilihusu; umuhimu wa vitabu na namna ya kuchagua kitabu, na mada ya pili ikahusu njia salama zinazo changia kuzingatia masomo, na jambo la mwisho zikazungumziwa faida za kiafya na kielimu anazo zipata msomaji.

Baada ya hapo mkuu wa maahadi ya Qur’an katika kituo cha Swidiqa Twahira akaongea kua: “Tumezowea kuona mambo mapya na mazuri kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kipindi cha miaka miwili iliyo pita wamekua wadao muhimu wa kuibadilisha jamii kupitia vitabu, hii ni njia muhimu ambayo inasaidia kutatua changamoto nyingi tunazo kumbana nazo katika kipindi hiki”.

Naye Dokta Asraa Abadi akasema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu sio kwamba imejikita katika jambo moja peke yake, bali wana angalia na kusaidia kutatua changamoto katika kila sekta na kwa watu wa tabaka zote, kwa maoni yangu; naona sababu kubwa za kufanikisha kwa ratiba hii inatokana na kuchagua mwandishi mwenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha maoni”.

Hafla ikahitimishwa kwa ufunguzi wa mtandao wa kieletronik, pamoja na kuzindua aprication za sim za kisasa (smart phone), na kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la mahdawiyya na washiriki wa ratiba ya marafiki wa maktaba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: