Haya ndiyo yaliyo pendekezwa na washiriki wa kongamano la kielimu kuhusu maktaba na maendeleo endelevu hadi mwaka (2030)…

Dokta Ammaad Maraiy Hassan
Baada ya kumaliza nadwa ya kielimu iliyo chukua siku mbili, washiriki walijadili mambo mbalimbali kuhusu nafasi ya maktaba na kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafikiwa ifikapo mwaka (2030), washiriki wa nadwa hii iliyo andaliwa na kusimamiwa na kituo cha faharasi na kupangilia maalumaati chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu wametoa mapendekezo yaliyo wasilishwa kwa niaba yao na Dokta Ammaad Maraiy Hassam kutoka wizara ya mipango ya Iraq, na hii ndio nakala ya mapendekezo hayo:

  • 1- Umuhimu wa kuwepo kwa mawasiliano baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wizara ya mipango ya Iraq, kwa lengo la kuhifadhi nakala kale na turathi za kitamaduni zilizopo katika orodha inayo fatiliwa na kamati ya taifa ya maendeleo endelevu, ili wizara ya mipango ipate fursa ya kuongea na wadau pamoja na wizara zingine kwa ajili ya kuunda kamati itakayo simamia mambo muhimu na kutoa misaada ya kipesa na kimkakati pamoja na kukusanya tafiti na kuzisambaza kwa taasisi zingine zinazo hifadhi turathi.
  • 2- Umuhimu wa kushiriki maktaba zote za Iraq katika kujenga nafasi ya nje ya Iraq katika sekta ya taasisi za elimu na za kuhifadhi turathi, kwani taifa linahitaji hatua hiyo ya kuwasiliana na ulimwengu wa nje, ili kupata uzowefu kupitia kuwasiliana na kushirikiana na mataifa yaliyo endelea na taasisi za kimataifa zalizo jikita katika maswala ya elimu na kuhifadhi turathi.
  • 3- Kuundwe kamati itakayo wajibika kufatilia utekelezwaji wa tuliyo taja, na Atabatu Abbasiyya iwajibike kuongea na viongozi wa serikali, kama vile wizara ya mipango, wizara ya mambo ya nje, na wizara zingine au taasisi za kiserikali.
  • 4- Kutoa wito kwa sekta ya sheria na watendaji kuhakikisha lengo la nne miongoni mwa malengo kumi na moja, linalo husu: “Kuongeza juhudi kwa ajili ya kulinda turathi za kitamaduni na kuzihifadhi”. Kupitia kutengeneza ushirikiano wa kieneo na kimataifa, pamoja na ushirikiano wa wawakilishi wa maktaba zilizo chini ya kamati ya taifa.
  • 5- Atabatu Abbasiyya iunde kamati maalum itakayo kua na jukumu la kuwasiliana na serikali kama ilivyo elezwa katika namba (1-3).

Mwisho wa kikao zikatolewa shahada kwa baadhi ya washiriki wa nadwa, pia kikao hiki kilihudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: