Waziri wa elimu ya juu asisitiza kua wizara inajali kuteua wahitimu walio faulu na kutapa shahada za juu zenye ufaulu mzuri…

Maoni katika picha
Waziri wa elimu ya juu na utafiti Dokta Abdurazaaq Issa amesema kua, wizara inathamini sana kufanya kazi na wahitimu vyuo vikuu walio faulu na kupata shahada za juu zinazo kubalika kimataifa, na akatoa wito wa kufahamu mazingira yetu, na mazingira ya taifa yaliyopo baada ya vita, tunategemea kuwa na wakati muafaka wa kuteua nguvu kazi hii ya pekee.

Aliyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya mwisho wa mwaka ya kutoa zawadi kwa wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq wa mwaka wa masomo (2016 – 2017) kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.

Akaongeza kusema kua: “Leo tumekunata sehemu hii tukufu kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walio hitimu na kufaulu kutoka vyuo vikuu vya serikali na binafsi hapa Iraq, walio fanikiwa kutekeleza malengo yao ya kielimu na wako tayali kutumikia taifa letu, pamoja na yaliyo fanywa na wizara ya elimu ya juu na utafiti, hakika imefanikiwa kufikisha ujumbe wake wa kielimu ulio zuia kuingiza elimu katika migogoro ya kivita, kisiasa na kivyama, kutokana na imani kua sekta ya elimu iko huru na haihusiani na mambo hayo, na kujenga kizazi chenye elimu bora, maadili mema na kinacho enzi utamaduni, kisicho kua na ubaguzi”.

Akabainisha kua: “Wizara ya elimu ya juu na utafiti inatilia umuhimu mkubwa swala la kujenga uhusiaano na ushirikiano na taasisi za elimu na utafiti kwa kufuata utaratibu wa vyuo vikuu vya kieneo na duniani kwa ujumla, jambo hili limekua na mafanikio mazuri pale vyuo vikuu tisa vya Iraq vilipo pata nafasi za juu za ubora katika vyuo vikuu mia kutoka katika nchi za kiarabu, na chuo kikuu cha Bagdad kilichukua nafasi ya kwanza kwa kua chuo cha (13) katika utaratibu wa mduara wa Uingereza”.

Akafafanua kua: “Hakika hali ya uchumi inaweza kuchelesha kamaliza miradi kwa muda uliopangwa, lakini hakuna jinsi lazima elimu ya juu ichukue nafasi yake katika jamii ya wairaq na taasisi za kitaifa za kiuchumi na kiafya pamoja na sekta zingine”.

Akasema kua: “tunashirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla ya kuwapa zawadi wanafunzi walio faulu, tunapenda kusema wazi kua wizara ya elimu ya juu na utafiti inapongeza sana swala hili tangu lilipo anzishwa, lakini kutokana na ukosefu wa hela na jinsi hali ilivyo kua katika kipindi cha (2017) imekua ni sababu ya kukwamisha kufanyika hili kwa ufanisi, mwisho aliwashukuru sana na kuwapongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutoa zawadi kwa washindi, nawatakia wote muwe na siku njema yenye taufiq na mafanikio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: