Maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka itifaki na umoja wa maktaba za kiarabu…

Maoni katika picha
Maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameweka itifaki ya kusaidiana na kushirikiana na umoja wa maktaba za kiarabu, kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano baina ya jumuiya na taasisi za maktaba katika nchi za kiarabu na kuinua uwezo wa watumishi wa sekta hiyo hapa Iraq.

Itifaki hiyo imesainiwa pembezoni mwa nadwa ya kielimu iliyo simamiwa na kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo isha hivi karibuni.

Itifaki imehusisha mambo yafuatayo:

  • 1- Hakika maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni mshiriki rasmi wa umoja wa maktaba za kiarabu za Misri katika kuandaa makongamano na kusambaza machapisho ya umoja huo.
  • 2- Kusaidia taasisi za nchini ziweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
  • 3- Kusaidiana katika kuandaa tafiti za kielimu kuhusu sekta ya maktaba na vitu vingine, na kufanya makongamano na nadwa.
  • 4- Kusaidia katika kutoa miongozo na mabango ya maktaba na taasisi za kitaifa na kieneo.
  • 5- Kushiriki katika kutoa maelekezo ya msingi ya utendaji wa maktaba na taasisi za elimu za kitaifa na kieneo.
  • 6- Kuwafanyia wepesi wa kushiriki wajumbe wa maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya katika makongamano ya kimataifa.
  • 7- Kubadilishana machapisho ya fani mbalimbali na aina tofauti.
  • 8- Muda wa itifaki ni miaka minne, na itaendelea moja kwa moja ikiwa hakuna upande unao taka kujitoa kwenye itifaki.

Upande wa umoja wa maktaba za kiarabu uliwakilishwa katika kusaini itifaki hiyo na kiongozi mkuu mtendaji Dokta Khalidi Halbiy, huku upande wa maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya ikiwakilishwa na Ustadh Faaris Adnani Hussein kwa niaba ya kiongozi mkuu wa maktaba Sayyid Nurdini Mussawi na kuhudhuriwa na Dokta Jasim Jarjis mmoja wa waanzilishi wa umoja huo na mjumbe wa kamati ya elimu ya umoja huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: