Yafahamu majina ya sifa (laqabu) za Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Jina la sifa (laqabu) kwa mujibu wa ufafanuzi wa watu wa lugha ni: Neno analo itwa mwanadamu baada ya jina lake halisi, neno hilo likamaanisha sifa au tusi na vinginevyo, hakika Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s) alikua anasifika kwa kila aina ya sifa nzuri, kila jila la laqabu alilo pewa lilikua na maana ya kumsifu na utukufu.

Hakuwahi kua na laqabu ya kumtukana au yenye maana mbaya, kwa sababu hakua na kasoro yeyote katika uhai wake, wala upungufu katika sifa zake, hadi maadui zake waweze kutumia mwanya huo kumwita laqabu mbaya na kumtukana kutokana na kasoro hiyo, kwa nini asiwe hivyo wakati yeye ni mtoto wa Imamu Kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na ni ndugu wa maimamu wawili wajukuu wa Mtume (s.a.w.w) na mabwana wa vijana wa peponi Hassan na Hussein (a.s), pamoja na ubora wa nasaba yake tukufu, hakika yeye alilelewa ndani ya nyumba ya wahyi na umtume, kafundishwa adabu njema na yule aliye fundishwa adabu njema na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), fahamu kua Mtume (s.a.w.w) naye alifundishwa adabu nzuri na Mwenyezi Mungu mtukufu, imepokewa kauli maarufu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Nimefundishwa adabu na Mola wangu akaniadabisha vizuri sana).

Ni wazi kua Abulfadhil Abbasi (a.s) amerithi utukufu na ukarimu kutoka katika asili yake, amepata adabu njema kutoka katika chimbuko lake, hivyo alikusanya sifa zote nzuri za umbo na ukamilifu, akawa ni chemchem ya utukufu na ukarimu.

Ndio.. hakika Abulfadhil Abbasi (a.s) ni kilele cha ukarimu na wema, tabia njema na adabu zake haviwezi kuelezeka, hivyo laqabu zake zimeashiria baadhi tu ya ukarimu na wema wake, zimejaribu kuashiria adabu na utukufu mwingi alio kua nao, tunazitaja kwa uchache kutokana na umashuhuri wa laqabu hizo kwa watu kama ifuatavyo:

Mlango wa Hussein (a.s).

Mlango wa haja (Babu Hawaaij)

Mnyweshaji.

Mnyweshaji wenye kiu Karbala.

Mwezi wa bani Hashim.

Mwezi wa familia.

Mbeba bendera.

Kamanda wa Alqami.

Kiongozi wa msafara.

Mlinzi wa wanyonge.

Simba mlinzi (sab’u qantwara).

Simba mkali.

Mja mwema.

Muabuduji.

Mrukaji.

Mshuhudiaji.

Msadikishaji.

Mfidiaji.

Mwenye kuathiri.

Mliwazaji.

Mlinzi na mwenye kuhami.

Mgongo wa wilaya.

Kiongozi wa jeshi.

Mustajaaru.

Mtekelezaji.

Mshughulikaji.

Mharakishaji.

Msafishwaji, na zinginezo nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: