Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa shindano la kisa kifupi kinacho elezea ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa wito wa kushiriki katika shindano la kisa kifupi kinacho elezea ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Sha’abi kitakacho andikwa na kutengenezwa kitaalamu kwa namna ambayo kitavutia wafuatiliaji.

Litakalo fanyika katika kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya tatu linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi).

Kamati imeweka kanuni na vigezo vifuatavyo vya ushiriki katika shindano hili:

  • 1- Maelezo yakidhi sifa za kitaalamu na kiubunifu kwa mujibu wa elimu ya visa vifupi.
  • 2- Kisa kielezee ushujaa wa wanajeshi au Hashdi Sha’abi kwa ujumla katika kulinda kwao taifa na misingi ya ubinadamu na maeneo matukufu, wala sio kumlenga mtu maalum.
  • 3- Kisa kisiwe kimesha wahi kutolewa au kuandikwa katika mitandao ya kijamii au kwenye kitabu au kimesha wahi kushiriki katika shindano lingine.
  • 4- Viandikwe kwa kutumia program ya (word) na kuhifadhiwa kwenye (cd) kisha vikabidhiwe katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu au kitumwe kwa barua pepe kwenye anuani ifuatayo (info@holyfatwa.com) pamoja na wasifu (cv) ya muandishi.
  • 5- Mwisho wa kupokea ni (21 Juni 2018).
  • 6- Nakala tano zitakazo shinda zitaandikwa kwa gharama ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Washindi watano wa mwanzo kila mmoja atapewa zawadi ya pesa ya dinari za Iraq (200,000) laki mbili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: