Atabatu Abbasiyya tukufu yashirikiana na watu wa mji wa Dabuni katika kongamano la saba la mwisho wa mwaka la kukumbuka kifo cha kishahidi cha Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshirikiana na watu wa mji wa Dabuni katika mkoa wa Wasitwa katika huzuni zao za kukumbuka shahada ya mama wa baba yake (Ummu abiha) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kupitia kongamano la Shahada ambalo hufanywa kila mwaka kwa kuratibiwa na idara ya Mawakibu Husseiniyya na kituo cha kitamaduni cha Zaharaa cha mji huo, chini ya kauli mbiu isemayo: (kutokana na jihadi ya Zaharaa (a.s) na damu za mashahidi wa fatwa ya jihadi ya wanazuoni Iraq imeshinda), kongamano hili limefanywa kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kongamano limefanyika siku tatu na lilikua na ratiba mbalimbali, ratiba ya ufunguzi ilihudhuriwa na ujumbe ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kundi kubwa la watu wa mji wa Dabuni na miji ya jiraji. Muwakilishi wa Marjaa dini mkuu Shekh Swalehe Qurah Ghauli alizungumza kuhusu utukufu wa bibi Zaharaa (a.s), kisha akaelezea kazi kubwa iliyofanywa na wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, pale walipo itikia mwito wa Marjaa dini mkuu wa kuilinda Iraq na maeneo matukufu, ambao wameweza kuzuia shari ya magaidi wa Daesh walio taka kuvuruga nchi, lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na juhudi zao zinazo tokana na bwana wa mashahidi (a.s) walifanikiwa kupata ushindi, akasisitiza kua damu iliyo mwagika katika ardhi hii itaendelea kua nuru ya uongofu kwa vizazi vyote.

Hafla hiyo ilipambwa na qaswida za mashairi zilizo zungumzia utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) na dhulma alizo fanyiwa baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kisha kikundi cha watoto kikaimba kwa huzuni kubwa, baada yao kikosi cha Nabau Adhim kikaonyesha igizo walilo lipa jina la (kuingia motoni).

Kongamano hilo lilihusisha maonyesho ya vitabu, ambapo kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kilikua na ushiriki mkubwa kwa kuonyesha machapisho yake na vitu vingine, maonyesho hayo yalidumu siku tatu, yamesifiwa na kila aliye yatembelea, na wameomba jambo hili lirudiwe tena siku zijazo kutokana na umuhimu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: