Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza ujenzi wa shule ya wanawake katika wilaya ya Hirah…

Maoni katika picha
Kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza kwa mradi wa ujenzi wa shule ya dini ya wanawake katika wilaya ya Hirah mkoani Najafu.

Makamo rais wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi (Samiri Abbasi Ali) ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu mradi huu kua: “Idara zote za kitengo cha usimamizi wa kihandisi zinashiriki katika mradi huu (Idara ya taaluma, idara ya ujenzi, idara ya viyoyozi na idara ya umeme), eleo la kiwanja linaukubwa wa (mita 825.5), jengo litakua na kumbi (16) kumbi (6) zikiwa ni za kusomea, na chumba kimoja cha ofisi na kingine cha walimu wa kike na sehemu ya vyoo, halafu kuna sehemu ya kulelea watoto na ukumbi wa minasabati na sehemu maalum ya mapokezi, mafundi wameanza kazi ya kujenga kwa kutumia vyuma, wanakata madarasa ba kuweka paa kwa kutumia panel za sandawich”.

Akaongeza kusema kua: “Jengo la shule litakua la ghorofa moja litakalo jengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita (5250), litakua na huduma zote muhimu, limesanifiwa na kupangiliwa kwa umakini wa hali ya juu, na lina utaratibu maalum wa sistim ya umeme inayo endana na sistim ya viyoyozi kwa mujibu wa ujenzi wa kisasa”.

Tunapenda kusema kua mradi huu unatekelezwa chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, umesha kamilika karibu asilimia (%88) bado kazi inaendelea hadi mradi wote utakapo kamilika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: